Thursday, December 9, 2010

Mungu, ubishi kati ya Kristo na mtume mohammad

tukiangalia dhana ya Mungu huwa inakuwa tofauti na kuleteleza dini kibao ambapo hata dini hizo huwa hazijibu suala hilo la Mungu.

ukristo na Uislamu hubishana juu ya Mungu. wengine huchenguliwa na Yesu Kristo kujiita mwana wa Mungu huku akimuita mungu kuwa ni baba na hivyo wafuasi wa ukristo woote kumwita baba, lakini wanasema ni kwa njia ya Kirsto tu mtu atafika kwa baba

waisilamu wao humwona Mungu kuwa sio Mungu ila ALLAH au MWENYEZI MUNGU, hawaoni kuwa ana undugu wowote wa kibinadamu na kwa hiyo hawezi kumzaa mtu yeyeyote japo ana Mtume atumwaye

wote wako sahihi kwani ukimtuma mtu waweza kumwita mwanao hata kama hujamzaa, hapa ishu ni kufikisha ujumbe, ni kutumia nadhalia kuwa huyu ni mtume au ni mwana wa Mungu ili tuweze angalau kupata idea ilivyo

huko asia kuna jamaa aitwaye Kabir, yeye humwita Mungu mpendwa wake (My beloved) lakini pia humfananisha na upendo wa mama na hivyo humwita my mother.

majina haya yote ni kwa sababu ya kukosa maneno halisi ya kumwelezea Mungu na hivyo kujaribu kufananisha ki-binadamu

ila kumbuka dini zote hutwambia kuwa Mungu yumo ndani mwetu na njia ya kufikia ipo ndani mwetu, hapa ndo somu huwa gumu vya kutosha kulielewa

maana tunatamanishwa kumwona Mungu as if anaonekana kwa macho haya madhaifu ya Nyama, kumbi ni kwa jicho la roho na kwa njia ya meditation, uzingativu

tutaona hasa juu ya Mungu

3 comments:

SIMON KITURURU said...

``Man made God in his own image..."
— Eckhart Tolle

chib said...

Watu wote wanavuta kamba kuelekea kule walipo. Mungu ni huyo huyo mmoja, hata watu wakijaribu kumueleza kwa mvuto wa kivyao kama ni wa kibiashara au kukomboa watu.
Mimi nahisi Mungu "ameumbwa" na wanadamu ili kupunguza vurugu na kuwafanya watu wajiheshimu na kuishi kwa amani au.....:-(

emu-three said...

Kwakweli Mungu ni huyohuyo mmoja, hakuna mungu mwingine, ila kila mmoja anatafuta jinsi gani ya kumuelezea. Yeye kawatuma wajumbe wake ili tumuelewe...tatizo linakuja hapo `kumuelewa' ...kwanza kumkubali huyo mjumbe ni issue...! Sio kumkubali kumuelezea huyo aliyetumwa nako imekuwa kazi kwelikweli...!