Tuesday, December 21, 2010

ni msimu wa sikukuu, sherehe lukukini msimu tena wa sikukuu wa kusheherekea kwa kula mapilau , kulewa na anasa kibao. ni mwisho wa mwaka wa kuona vituko vya hapa na pale.

swali lilikuwa likinisumbua mimi nitasheherekeaje? situmii vilevi wala mapilau wala nini na nini tena, lakini ni somo la ubinadamu wa kweli aliokutana nao matondo ndio unaonipa jinsi ya kusheherekea mwaka huu
mimi na maiwaifu tutatembelea hospitali moja na kuwaona wagonjwa na kuwapa pole kwa maneno ya kuwatia moyo. badala ya kupeleka pesa kwa pasta au padri au nani sijui, sisi kidogo chetu tutaenda hospitali, kwa wahitaji wa kweli ndipo tutakapomalizia sikukuu na sherehe zake

shukrani kwa matondo kwa kutufundisha umuhimu wa kuwajali kwa kuwakumbuka wahitaji wa kweli