Monday, December 20, 2010

ni mwaka wa ndoa, ni nzuri ni sanaa


tarehe kama ya leo mwaka uliopiti nilijikuta nikifunga ndoa ya kiserikali kupitia KKKT. nilikutana na Omugonzibwa wangu juni 6 mwaka 2008 na siku kama kumi baadaye tukaamua kufunga ndoa ya hiyari au ya kivyetu vyetu


sasa katika kubadilisha ajira tukajikuta tukilazimika kufunga ndoa ya kanisani/serikali. kwa mwaka huu wote uliopita nimekuwa nikijifunza na nimengundua ya kuwa ndoa ni shule lakini pia ni sanaa


lazima mkoseane ili upendndo uongezeka, lazima kuheshimu misimamo ya mwenzako, lazima kusaidiana kwa vyovyote na kuna wakati unalazimika kufanya kile ambacho hukujisikia kukufanya wakati huo ili tu kushirikishana na mwenzio


ukiingia kwenye ndoa kwa lengo la ndoa na kama unafanya uchaguzi imara wa kwako na sio wa wazazi wala jamii, ndoa inakuwa ya maana na yenye furaha lakini ukiingia kinyume na haya basi hufui kuingia na kamwe haitakuwa ndoa


basi yafaa ndoa hiwe ni ya kwako na sio ya kijionyesha. muwe masikini au tajiri ndoa itakuwa diri na mtaishi kwa amani


ni mwaka kamamili japo kiuhalisia ni zaidi ya miaka miwili

8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

HONGERENI SANA!

Mija Shija Sayi said...

Hongereni sana, ni kweli ndoa ili iwe ndoa ni lazima iwe ya kwako na si ya kujionyesha. Nimeipenda sana hiyo pointi.

Mbarikiwe sana.

emu-three said...

Wengine wanasema NDOA NI NDOANA, IKIKUNASA HUNASUKI, UKINASUKA UNA MAJERAHA. Na kuna mmoja kasema ndoa ni kaburi la mapenzi...ukiyasikia hivi kama upo nje ya ulingo utasema mmmh, jamani humo ndani ipo kazi nitaweza kweli.
Lakini hili sio kuwa kila mtu itakuwa hivyo, kama waliotangulia walivyosema kuwa ndoa ni kati yenu wawili, wakuijenga ni mume na mke na wakuibomoa na hawohawo! Akili kichwani mwenu
HONGERENI SANA, NA TWAWAOMBE MOLA AWABARIKI NDOA YENU IWE YA AMANI NA UPENDO!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hongereni jamani!

Anonymous said...

Ndoa ili iwe ndoa ni lazima iwe ya kwako na si ya kujionyesha. Nimeyapenda maneno hayo na yamenikuna kweli.
Hongera sana Kamala

Mzee wa Changamoto said...

Hili ni funzo kuubwa saana.
Niliwahi kunukuu kwenye SURAKITABU kuwa "harusi zote hufanana na ndio maana hata wafungishaji hukariri jinsi ya kufungisha, lakini kila ndoa ni ya kipekee" Tunaona namna ambavyo watu wanaia KUISHI MAISHA YA NDOA KAMA YA BABA ZAO, AMA MAMA ZAO AMA NDUGU ZAO
Hakuna ndoa inayojirudia kwa kupangwa. Matukio yatajirudia kwa kuwa yameletelezwa kujirudia kutokana na miongozo ya waishi
Lakini kama ulivyosema, ILI NDOA IWE NDOA NI LAZIMA IWE YAKO NA SI YA KUJIONESHA.
Labda ambalo tunashindwa kutambua ni kuwa SIRI NYINGI, KUBWA (NA PENGINE) ZOTE ZA MAFANIKIO YA NDOA HUBAKI KUWA SIRI.
Kijengacho ndicho kibomoacho, hivyo kukiweka wazi ni kujibomolea ujengapo'Blessings kaka. Hongera kwako na kwa wapendwa waifanyayo familia yako iwe yaki

Anonymous said...

maneno yako yamenigusa, niliingia kwenye ndoa kwa kufurahisha wazazi na ndoa hiyo baada ya miaka sita ilikuwa ndoano. maana haikuwa ndoa yangu ila ya kujionyesha kwa wazazi

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

anony, labda inagusa lakini mimi nilijifunza kutofanya makosa haya kwa kuangalia ndoa ya marehemu baba yangu.