Monday, December 13, 2010

uhalisia au maana ya Mungu

 Katika mjadalaa wa kile tukiitacho Mungu a.k.a sir God na majina mengine, kina mtizamo mwingine na labda ambao ni chanya zaidi 

Kiuhalisia twaweza ungana na wanasayansi asemao ni nguvu tu, wao wanatambua uwepo wa nguvu tu ambayo wanasema haiwezi kuharibiwa wala kupindishwa, lakini wanashindwa kutwambia jinsi ya kuifikia na kuifaidi nguvu hiyo na hivyo basi dini huingilia kati kwa mikwara juu ya nguvu hiyo, lakini suluhu hapa ni ile sayansi ya roho (science of the soul)

Twaweza iita nguvu kuu (supreme being), lakini kama sisi ni uwepo (being) basi yenyewe ni Bonge (supreme) la uwepo.

Kama sisi ni roho (Soul) basi yenyewe ni roho kuubwa (over soul /supreme soul).

Mfano wa nguvu hii na ubainadamu wetu hufananishwa na maji kwamba Mungu ni bahari na sisi ni tone la maji na kwamba tone hili likijiunga majini basi huwa kitu kimoja na bahari na kamwe huwezi kutenganisha tena vitu hivi

Lakini je twawezaje kuwa kitu kimoja au umoja wetu uko wapi au tumfikieje Mungu?
Swali hili laanzisha mada juu ya Meditation


1 comment:

emu-three said...

Mhhh Mkuu, hili swala la kiimani, na watu wengi wanajikwaa kila wakitaka kwenda huko, kudadisi `huyu mungu ni nani~'
Mhh, bwana, uhalisia wa mungu hauelezeki, mungu ni kila kitu, na huwezi kumfananisha naye au kumlinganisha naye ili awe sawasawa na yeye...utafikia sehemu utajikwaa..!
Ni hayo tu!