Saturday, December 18, 2010

ukweli, amazima, The truth

ukweli ni jambo linalosemakena lakini limekuwa gumu sana katika maisha haya tuishiyo wanadamu, kile kiitwacho uongo sasa kimechukua nafasi ya ukweli.

katika jamii zetu kuna kila mbinu ya kupeleleza na kujua ukweli lakini nazo uishia kuwa uongo, tuna taasisi kibao za uchunguzi ambazo nazo zimekaa kiuongo

tukija kwenye ulimwengu wa roho kristo anadai kuwa mkiijua kweli nayo itawaweka huru kwamba ukweli na uhuru vinaenenda pamoja au ni kaka na dada kama sio mume na mke

ukweli unafananishwa na haki, ukweli unaleta kujiamini, kuna wanaodai kuwa Mungu ni sawa na kweli na kuwa sisi pia ni sehemu yakweli

1 comment:

SIMON KITURURU said...

Uongo ni misingi ya ukweli!:-(