Tuesday, January 18, 2011

ajali ya piki piki, sitaki tena

nikiwa naendesha pikipiki kuelekea nyumbani kwangu nilijikuta nikidondoshwa na pikipiki hiyo. kutokana na ugumu wa usafiri na kutaka kujitawala nilikuwa namalizia mipango ya kumiliki pikipiki binafsi, ila nikijiuliza changamoto za mvua, vumbi nk nitazimaliza vp,

kabla ya kupata jibu la changamoto hizo najikuta na changamoto nyingine kubwa, ajali, nimedondoka na pikipiki. huwa naendesha mwendo wa taratibu nakumbuka situmii vihamasisha mwili vinavyoweka akili pembeni katika maamuzi yapasayo kuwa ya busara

nakata kona (napinda kona? kipi kiswahili sawia?) kuelekea nyumbani kwangu, naona miujiza na kudondoko, naambiwa eti wingi wa changarawe ndo umeleta soo, mtu sikimbii?

sikupata majeraha makubwa na sjambo, ila mpango wa kumiliki pikipiki binafsi na ufe kuanzia leo

5 comments:

emu-three said...

USITUKANE wakunga na uzazi ungalipo mkuu. Kabla ya yote pole sana. Hiyo tunaiita ajali kwani hata kama ungekuwa ukitembea na TZ 11, ungeweza kujikwaa, na kuanguka na hata kuteguka kiuno, ...
Usikate tamaa, zote ni ajali tu!

Hebu soma hii: http://miram3.blogspot.com/2010/05/bodaboda-na-mwendo-wa.html

Na ukimaliza hiyo soma pia hii:
http://miram3.blogspot.com/2010/11/haraka-haraka-haina-baraka.html

Yasinta Ngonyani said...

Pole Kamala kwa kudondoka na pikipiki. Ila kama alivyosema em3 usiseme kamwe.

Anonymous said...

KAKA POLE KWA AJARI.
SIKUUNGI MKONO KWA UAMUZI WAKO WA KUACHANA NA PIKIPIKI. KWA MAZINGIRA YETU YA BUKOBA PIKIPIKI NI YA MUHIMU SANA UKIZINGATIA KUWA INAKUWEFESHA KUFIKIA MAENEO MENGI AMBAYO MAGARI HAYAWEZI KUFIKA, ACHILIA MBALI CHANGAMOTO ZA VUMBI NA MVUA.
BADILI UAMUZI BROTHER

NI KAWAMALA. A

Goodman Manyanya Phiri said...

Unataka ununuwe gari? Mbona wanasema magari ndio yaathiri mazingira yetu kama binadamu?

Pole sana, Rafiki yangu. Lakini Wahenga waliwahi kusema (hapo kama nawanukuu Kiswahili chema):


"USIACHE MBACHACHA KWA MSALA UPITAO."Kwa hiyo, pikipiki ni yako tu, anguka usianguke; na ukishindwa napikipiki tembea tu kwa miguu na hapo hutaanguka kabisa labda kama umelewa; na kama hujalewa utajikwaa tu kwisha vidonda vyake hupoa baada ya siku chache tu!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ushauri nitauzingatia