Friday, January 21, 2011

"BUSU"

binadamu na ubunifu, unaweza kujiuliza mtu aliyegundua Busu alikuwa anafikiria nini au anafanya nini mpaka akaja na ugunduzi huo. sasa ni fasheni kubusiana!

ila sasa lengo la busu ni kisaikolojia zaidi hata kama ulitaki. najiuliza maswali mengi juu ya abusiwaye kama kweli anaitamani hiyo busu au analazimika kuipokea maana haibishi hodi

nikiwa nakabusu kamrithi kangu huwa sielewi kama kanafurahia busu hilo achilia mbali kutoelewa maana yake. nakumbuka nikiwa bado kajitu kadhuchu marehemu baba yangu alikuwa na tabia ya kunibusu. kakweli nilishindwaga kumzuia kwani busu lile lilikuwaga shida kwangu. yaani alivyokuwa amenyoa ndevu basi mashavu yangu yalichomwa na ndevu hizo na kufanya busu kuwa kihama

je mimi ninapokabusu kamrithi kangu kweli kanafurahia mashavu yale kweli?

uzuri wa busu uko kwenye busu lenyewe au kisaikolojia zaidi?? najiuliza
may the gloom kiss the bride!

5 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Tungali watoto, wazazi wetu wanatubusu ila tuzowee (hapo baadaye ukubwani) kuwabusu wake au waume zetu kama FOREPLAY au kitendo cha kutanguliza tendo la kupeyana mimba.


Busu ni sehemu moja ya SEX. Na SEX ni sehemu moja ya upendo wa ndugu, nchi yako hata na upendo wa Mungu wako! Maisha bila busu simaisha ya binadamu. Na busu halikugunduliwa na mtu yeyote, bali sote ni watoto wa busu. Na tumefanya kosa kubwa sisi binadamu duniani kote kwamba hadi leo hamna hata jiji moja liliopewa jina la "Busu" ikiwa huku mama zetu karibu wote walishika mimba kutuzaa sisi baada ya kupigana busu na baba zetu!

Yasinta Ngonyani said...

Ndiyo Kamala! Busu, sijui kama kakijana kako kanafurahia libusu lako. Kama alivyosema kaka Manyanya inaweza ikawa busu kwa mke na mume kwa kutaka kuwa karibu au niseme tendo la ndoa na pia unaweza ukambusu kaka, dada, rafiki nk. Duh! Kamala nawe?!!!!

emu-three said...

Yah, busu...mmmh, busu ni sehemu ya `tendo la ndoa' mmmh , ok, labda natizama undani wa busu zaidi.
Busu ukilichukulia kama `salamu' ya kushikana mkono itakuwaje, kwasababu wengi wakiowashika watoto wanawaambia, nibusu basi...mwaah! Je ni tendo la ndoa?
Jamani najiuliza tu, kwani busu huenda lina namna nyingi...ila swali kauliza ni nani aligundua hili tendo...!

SIMON KITURURU said...

Nahisi KISWAHILI ni kugha dhaifu na haina misamiati mingi!:-(Busu kwani ni nini?

SI nasikia kuna wadaio kula mate ni busu?:-(

Nawaza tu kwa sauti!:-(

Tandasi said...

haha busu ni busu