Wednesday, January 19, 2011

gafra wewe ni mfanya maamuzi mkuu

ulizoea kuamuliwa hata ngua ya kuvaa, chakula, malazi na hata muda wa kulala

ila sasa mambo hubadilika na unajikuta wewe ndo mwenye kufanya maamuzi ndo bosi na ndo mkuu

ila sasa kufanya maamuzi ni kitu kigumu na ndio maana huwa tunaamua kuwachagua viongozi wabovu, kusoma masomo magumu, kula chakula kisichotufaa na kuingia kwenye ndoa zitakazotusikitisha

mara nyingi huwa tunajutia matokeo ya maamuzi yetu

ila unajikuta wewe ni mfanya maamuzi mkuu, nyumbani, ofisini au kwenye ishu kibao,

angalia matokeo ya maamuzi yako, ila nakusihi usilie

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Mmmmhhh ! kufanya maamuzi ni kweli si jambo rahisi. utakuta mtu hata kuamua avae nini anashindwa lakini kama angakuwa na nguo moja nadhani maamuzi yasingekuwa kaaazii. naacha....