Wednesday, January 26, 2011

ilitokea jamaa akamuuliza mshikaji wake kuwa bibi yake ana umri wa miaka mingapi na yule mwenzie akamjiba kuwa atakuwa na umri wa miaka 8o, basi jamaa akamjibu kuwa yawezekana huyo ashajaza choo cha kwake pekee!

Labda kilikuwa ni kichekesho na kijembe kwa jamaa yule kilicho nipelekea kutafakari na kujiuliza juu ya kula na kujisadia. Nimejaribu kuhesabu chakula nilichokwisha kula mpaka sasa hivi labda duh ni aibu

Kuna wakati niliweza kula kama kilo nne kwa siku hivi labda milo yangu yoote ya kila siku ni kama kilo moja kamili hivi. Ila sasa ukipiga hesabu ya chakula nilichokwisha kula mpaka sasa, mzee unapata kama tani ishirini na tano, yaani kama mafuso mawili hivi ya chakula yamewahi kuingia tumboni mwangu!! Ni noma

Sasa usijiulize choo, sijui itakuwaje ikikushanywa haja zote nilizo kwqisha ziporomosha kwa kujifungia chooni au porini ni kiasi gain, nafikiri inatengeneza mlima, hebu jaribu basi na wewe kuhesabu chakula chako tangu uje diuniani, ni aibu!!

Mwili haujengwi kwa matofali


4 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Ni aibu kweli. Lakini nimewahi kwangalia toleo mmoja la huyu bibi tajiri waKimerikani Oprah Winfrey pale aliposema sukari tunaonunua madukani ikiingia katika mishipa ya damu ni sawasawa na chupa zilizosagwa na akaanza kutonyesha magunia ya sukari tunayotumia maishani mwetu ili kusababisha dalili za ugonjwa wa kisukari.

Hata hiyo miaka 80 hatufikii namna hiyo. Afadhali bibi yake Kipenzi!

Asante Rafiki kwa posti yenye vichekesho na kufundisha!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

karibu

emu-three said...

Unakubali kuwa `kula na kunya, na kula ni mzunguko. Yaani unapokula, chakula huja kugeuka mavumbi, ynayokuwa mbolea, ambayo ni chakula cha mimea, inayozalisha chakula...ndio hivyo mkuu, usijali sana!

SIMON KITURURU said...

DUH hii kali!:-)