Friday, January 14, 2011

kuchokana maishani au maisha ni kuchokana

maisha yetu yna kanuni mbali mbali, tuna uhitaji wa vitu na watu mbali mbali kwa nyakati tofauti kuanzia mwanzo hadi mwisho. lakini mwisho wetu huwa ni mbaya wa kuchukia karibia kila kitu na hata labda kujichukia sisi wenyewe

ili tuweze kuja duniani tunahitaji kuishi tumboni mwa mama zetu japo mwanzo kabisa tunahitaji watu wawe na tamaa ya kufanya tendo la ndoa, baada ya miezi tisa, twalichoka tumbo la mama, twataka kuzaliwa, basi tuzaliwapo, tunamhitaji sana mama, upendo wake na mwili wake ndio chakula chetu

tukikua tena, tunahitaji vitu vya kuchezea (toys), tunahitaji marafiki wa utotoni lakini baada ya muda, twavichoka tena. tukikua twaona umuhimu wa baba, analipa school fees huku mama akitupatia chakula bora na malazi mazuri, twawahitaji sana


twakua tena na kutaka kueleza mawazo yetu, basi twahitaji marafiki wa kupiga nao story, hisia na hasa mihemko yatutawala, twahitaji wa kuituliza, ni mpenzi wa kufanya naye mambo ya gizani, wagundua kumegewa sio tamu, basi wahitaji mwenza wa kumaliziana naye kila kukicha, then wagundua hisia sio dili au mwenza kabadilika uzuri, then watafuta watoto, wanavutia na wanapendeza

wagundua kuna hatari, wajihusisha karibu na dini, then watoto nao kero, wanataka huduma kibao, karo, chakula nguo nk, unaanza kuhitaji mfanyakazi kwani watoto hawakusaidii, then wazeeka wahitaji kuwa karibu na viongozi wa dini, unawapa sadaka hawakusaidii sana

umezeeka, kwa ufupi umeichoka dunia, umeuchoka mwili wako na unatamani kufa japo unaogopa jinsi ya kufa

kwa hiyo tunaishi kwa kutamani na kuchokana

1 comment:

SIMON KITURURU said...

Si utani Mkuu!Maisha kiboko!