Thursday, January 13, 2011

polisi wa Tanzania na kudhibiti wema kuwaachia huru majambazi


kuna maamuzi ya kisiasa ya ajabu juu vyombo vya ulinzi. awali ya yote mimi ningependa kuona mapolisi na wanaoitwa wana usalama wengine (sioni kama ni wanausalama kwani wanatmia vifaa vya uhasama zaidi) wakilinda maslahi ya umma badala ya wanasiasa wachache tunashuhudia mauaji na vipigo vya polisi.

ni kule Arusha wengine wamekufa na wengine kujeruhiwa vibaya, Dar nako Cuf walioandamana walikutana na chamtemakuni, wanavyou nao ni marungu, viboko, maji ya washawasha, mabomu ya machozi na risasi za moto mpaka watu wanapata vilema vya kudumu na vifo
polisi yetu inawavamia na kuwachabanga raia wanaotaka kueleza hisia zao kwa amani na kusababisha vurugu huku ikiwaachia majambazi wakitesa!

tuachane na mafisadi kwanza, ila wateka magari na wauza Unga wanatesa na kufurahia maisha huku raia wakitwangwa na polisi ipasayo kuwalinda


kama unasafiri kwa gari kuelekea Bukoba, ngara au Kigoma, saa kumi na mbili jioni hauruhusiwi kuendelea na safari na ni lazima ulale njiani. mara nyingi mabasi husimama kahama, bihalamro au eneo la mizani, kisa cha kusimamam na kulala njiani ni majambazi hatari, wanatawala na wanaizidi serikali/polisi nguvu ndio maana raia wema wanalazimika kulala njiani ili majambazi watawale
kwa tafsiri ya haraka majambazi wanatawala maeneo hayo.

lakini polisi wako bizi na kuwa twanga raia wema, wasio kuwa majambazi wala wezi
nafikiri ifike hatua polisi na majeshi yetu yoote walinde Umma na sio wanasiasa au vyama vya siasa

2 comments:

chib said...

Toleo hili limenikuna sana!

Goodman Manyanya Phiri said...

Zote hizo ni kazi za polisi. Si vema polisi wa nchi yoyote kutumia ukatili wowote. Lakini sivema tena polisi wafanye kazi moja waache zingine; hivyohivyo itakuwa kosa wakiangalia majambazi pekee yake waache kwangalia maandamano yanayoweza, kwamfano, kuleta hatari katika usalama wa taifa.


Labda, Mwandishi-mwenzangu, ungefanya vema kwandika posti mbili tofauti: moja kuhusu majambazi yanaotawala kwenye sehemu ulizotaja. Yapili posti iwe kuhusu ukatili wa polisi.