Friday, January 28, 2011

tatizo la kutembelea vijijini kwetu, mi bishoo la tauni

natokea kijijni kanyigo, tatizo la kutembelea vijijini kwetu huku bukoba ni shibe waliyonayo wanakijiji kwamba wana chakula cha kutosha. kila nyumba unayoingia unapikiwa chakula na kula. ukikataaa kula unaonekana hufai au mchawi kwa hiyo ni lazima upata msosi ni kilaji ambacho ni lubisi au akakonyagi na siku hizi watu wameendelea hasa wa kule kanyigo, kitu ni bia tena ya baridi

ila sasa mimi naonekana bonge la bishoo, siri Nyama, siri mayai wala kutumia kilaji cha aina yoyote basi naonekana sijui limtu gani sijui, bishoo harafu naonewa huruma wakati mimi pia nawaonea huruma wanaokula vile nisivyokula mimi!

ni noma, unakula mpaka basi, vijiji vyetu bwana!

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Huko ni safi na huu ndio utamaduni wetu sio unaenda sehemu unaulizwa kama una njaa. Lakini Kamala unaweza kula ugali bila nyama au mayao au ndizi tu au wali tu:-)

Goodman Manyanya Phiri said...

Usitumie gari wala baskeli wala chochote unapokwenda vijijini: nenda kwamiguu... tena ikiwezekana utembelee nyama kabisa bila kiatu wala kandambili!

Utakuja kuwashukuru wote wale wanaokupa miugali na nini nanini. Tena hutabagua na kusema nakula hiki naacha kile... njaa hiyo, Rafiki yangu!

Kama kaka-mtu niruhusu niseme: "Mkataa pema pabaya panamwita".

chib said...

Kamala mtani wangu, mbona unaongea kikurya! Siri au sili

Mcharia said...

Bhita ni Bhita mura!