Monday, February 7, 2011

kijiwe hiki kifungwe kwa muda?

naona liwe swali kwa wadau kabla ya kuwa uamzi rasmi

naona kama ni wakati wa kuchukua lizkizo ndeefu ya kuacha kujivinjari kijiweni hapa. naona nifunge kijiwe hiki kwa muda wa kuanzia mwezi mmoja au mpaka mwaka au zaidi

sio kwamba niko bize ila naona kama nastahili likizo katika hili

naona nisimamishe kijiwe hiki kwa Munda mpaka hapo nitakapotaka kurejea tena,

au mwasemaje wadau? si ni uamuzi mzuri huu?

7 comments:

SIMON KITURURU said...

Mie nakataa wazo hilo!

Ila kwakuwa nahisi kuna kitu sijui ambacho muhusika ni wewe!

Nahisi hata tukatae vipi kama MAAMUZI ndicho ulichoamua, tutastukia tu hapa hutuhabarishi tena!

Nimetoka kwa Rasta LUIHAMU naona kaandika I hate Blogging, nakuja hapa naona Mkuu uko mguu ndani mguu nje!

DUH!

Labda tutonye zaidi kuhusu swala!La sivyo wewe usiache na uwe tu unatutonya kitu hata kwa uhaba ila kila tu uwezapo!

Si nasikia kwa atangaziaye watu anaacha ngono wakati huo ndio ofa za ngono huzidi?

Na si labda ukisha tutangazia unaacha kwa mwaka kesho yake ndio unaweza ukawa umezibua mambo kibao utakayo kublogu?

Yasinta Ngonyani said...

Wewe ni muamuzi lakini TUTAKUMISS SANA:-(

Goodman Manyanya Phiri said...

Likizo hiyo huiwezi nakwambia mimi! Kabla ya mwisho wa hata wiki mbili utajikuta umerudi tena mchakamchaka.

Jaribu basi!

Mcharia said...

Unatutegae!!!???

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Unataka tuandamane?

chib said...

Hii ni dalili ya ukata, maana mambo ya internet yanahitaji fweza. Acha visingizio vya kupumzika.
CCM Hoyeee kwa kutukausha mifuko na kutuelekeza uchumi wa Mabwepande

danie said...

unataka nafasi ukacheze na dogo?tumekustukia acha hizo