Friday, February 25, 2011

kuacha kublogu (kupumzika) na kutokuacha

ulikuwa ni uamzi wangu tu kwamba naona kama nastahiri labda kujipanga upya ili nijeupya au nikamilishe baadhi ya Mambo ili niweze kuwa kwenye mazingira fulani mazuri ya kublogu na hivyo badala yakuwa kimya tu nikaona niwashirikishe wadau.

majibu yao hayakuwa positive kwa wazo langu hadi wengine walitishia kuandamana, sijui kulekea wapi!

nikapokea emails na simu kutoka hata nje ya nchi kwamba nikifanyacho sio sahihi! na nikweli sio sahihi kwangu mwenyewe na kwa wale wanisomao

siwezi kukosa cha kupost kamwe mtu mimi mweye akili wazi ila niliona kama nastahili kujipanga upya

nitaheshimu woote waliopinga wazo langu kwa kuendelea kuwepo hapa japo kiaina mpaka pale nitakapo kuwa tayari ili kuwepo kwa kasi mpya (sio kama ya kikwete) ili iwe blogu bora kwa kila mtembeleaji

nawasilisha

2 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Kumbe ulitaka kurejea nyuma kidogo ili upate msukumo mpya kuja kupigana?

Hapo sasa nakuunga mkono. Hata kondoo dume anavyopigana anafanya hivyohivyo!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mimi nilikuwa nimepanga kuitisha maandamano makubwa ambayo yangeishia kwa Mwombeki ili kupinga mkakati wako huo....

Kama ungekuwa umefafanua vizuri lengo lako la kupumzika ni nini, pengine hata nisingekuwa na haja ya kuandaa maandamano.

Goodman - mfano wako wa kondoo dume umenifurahisha. Kweli wajua kukitumia Kiswahili!!!