Monday, February 28, 2011

maandamano!

kuna wanaodai eti kuandamana ni kupinga kitu fulani na haswa ya kisiasa kama yanayoendelea ulimwenguni sasa ni kupinga viongozi fulani kwa hali ngumu

ila hii kali, mimi nilipokuwa chuoni nilipata shida ya kununua chakula na kukosa 250/= ya daladala, sasa kule Libya wanavyuo wanamlalamikia Gadafi kwa kutokuwa jengea parking za mgari yao!! hii kali

kuna wanaodai maandamano haya yanamkono wa majasusi yanayotaka kuiba mafuta na kujinufaisha na vitu vingine!

wa-Libya wangejua wanachokililia wangeekuwa wapole, nawashauri waje Tanzania waone utajiri wa nchi unaozidi wa kwao, then waone umasikini wa wananchi wa Tanzania harafu walinganishe na Libya yenye mafuta tuu lakini wananchi matajiri then wamtukuze Gaddafi

vinginevyo wanakwepa mkojo kukanyaga kinyesi, watalia nakusaga Meno! (sijui kama wote wana meno)

2 comments:

SIMON KITURURU said...

Sasa ni nini siri ya WATANZANIA kuridhika hivyo na umasikini kitu kifanyacho inasemekana wanavumilia MAFISADI matajiri watawala ambao hawang'olewi kwa nguvu za walalahoi wawapao ulaji?

Goodman Manyanya Phiri said...

Kumradhi sana: naandika hapa haraka haraka. Sina muda wa kurudia na kusahihisha makosa ile ya kutosha, lakini@Simon
Nini tofauti katika yule aliyetoa kauli (EXPRESS HIMSELF/HERSELF VERBALLY) na yule aliyefanya maandamano?

Mimi ningesema tofauti ni kiwango cha elimu (LEVEL OF EDUCATION).

Pamoja na matatizo ya ufukara (A LOWEST PER-CAPITA-INCOME), naamini hilo taifa ni moja yake yenye elimu ya kiwango cha juu Barani. Na ndio maana mara nyingi wanaamini kauli ndio bora kuliko maandamano. Kumbuka tena kwamba katika maandamano moto unawaka na vitu vingi vinavunjwa na kuteketezwa ikiwa vyote ni vya wananchi walewale wanaofanya maandamano!

Nawazo kwa mawazo yangu madogo kwamba labda Mtanzania anaona maandamano ni ujinga tu!

Kauli ya Mtanzania nilidhania nilipofika mara ya kwanza Dar es-Salaam mwaka 1985 na nikamwona huyo mtu barabarani Temeke alivyokuwa anamtukana Nyerere kwa sauti kubwa.

Matusi kwa mheshimiwa yoyote wanchi yoyote duniani ni kukamatwa na polisi papo hapo. LAKINI YULE BWANA,NILISHANGAA, ALIENDELEA TU NA KUMPA TENA MAMA YAKE NYERERE MATUSI YA NGUO ZAKE ZA NDANI TENA KARIBU NA KITUO CHA POLISI LAKINI HAMNA POLISI HATA MMOJA ALIYEMKAMATA.

Basi mimi nikafikiri: "Mimi kweli nimekuja Tanzania kujifunza uhuru waMsouth-Afrika utakuwa kauli yake huru".


@Kamala

Nami naamini kabisa siyo wananchi wa Libya waliyoanzisha maandamano dhidhi ya Gadaffi, bali ni maadui zake wa kimataifa. Baada ya kuondolewa kwake Gadaffi Walibya watakuja kujuta.