Friday, February 4, 2011

nishati hapa tanzania hazishikiki

unaweza kujiuliza mengi kama wewe ni mtanzania anayeishi tanzania juu ya vyanzoo vya nishati. niliona jana kwenye TV nyumba moja iliyoungua kutokana na mshumaa na kutokana na kukatika kwa umeme jijini dar harafu ikaona tangazo la wizara ya maliasili linalotaka watanzania kulipia kodi mkaa

kwanza unajiuliza kuna kodi ngapi zinalipwa kwa vitu vya asili alivyotoa Muumbaji kwa watu wake na sijui kama mchomaji mkaa anautoa shambani kwake ni lazima alipie

kubwa zaidi hapa ni jinsi nishati za nchi hii zisivyoshikika, bei ya umeme iko juu achana na umeme wenyewe usiokuwepa au unaotetemeka mara mwingi mara mdogo mara mgawo. harafu uje kwenye maajabu mengine kama vile gesi ambayo upatikanaji wake ni noma na bei yake naomba nisiulizwe!

mafuta ya taa ndo maawee, kila niendapo kununua huwa nakuta yamepanda bei, then tegemeo ni kuni na mkaa, sasa mkaa unavikwazo vya kutosha lakini pia ni kodi sasa. najiuliza maisha ya mtz yakoje juu ya nishati?

heri yangu ninayeishi kijijini maana kuni na mkaa havina jamaa wa maliasili wala nini

sijui tatizo la watanzania liko katika kuchagua viongozi wanaotoa pesa, kofia, falana, kanga na pilau au ndo uhalisia

1 comment:

emu-three said...

Mkuu hoja kama hii ilitakiwa ijadiliwe sana, WABUNGE, waishilikie kidedea, kwani kwakweli `gharama za uendeshaji zinakuwa kubwa sana sababu ya `nishati' ...nina maana umeme na mafuta(diesel etc),
Tatizo la umeme, nashindwa kujua kwanini liisitwe janga...hebu angalia madhara kama hayo, mishumaa inaunguza vitu, lakini je tumeangalai atahari za mosho wake, athari za mazingira...
Angalia minguromo ya majenerata, masikio yetu sasa yanajaa ukungu, watoto wacahanga wanaozaliwa je hawaathiriki na hili?
Tunapedna kuangalia mambo juu, juuu, lakini kiundani athari za matatizo haya ni makubwa!
Tunaotumia LUKU, tunalaani sana, kwani tumeshalipa pesa zetu, wamzila, lakini huduma hawatupi, hawaoni kuwa wanatutendea sivyo-ndivyo?