Wednesday, March 2, 2011

eti ni sehemu za siri, siri ipi?

labda tunahitaji maelezo juu ya neno siri. kubwa zaidi ni juu ya zile ziitwazo sehemu za siri. hapa mtu humaanisha jinsia au kufinyiacho tendo la ngono

sijui kwa nini wale mizimu a.k.a wahenga waliamua kuziita sehemu za siri! sioni usiri wowote kwa ile maana jumla ya neno siri!

watu wote unaowaona ujue ni matokeo ya ngono harafu eti ni sehemu za siri (vifaa vya ngono).

ukimuona mtu hata avae baibui unajua kuna kitu ndani mle hata usipoona.

eti sasa ni sehemu za siri, siri ipina siri kwanani??

usiniulize kwanini wajifungia choooni na bafuni wakati hukimbizwi na jambazi wala simba! woga wa nini? siri ya nini hii???

4 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Hapo umeuliza swali nzuri sana. Labda ni siri kwa kuwa wapo wengine hawataki wajulikane kwa kila mtu kwamba wao siyo jinsia ile jamii inavyowadhania bali wanataka wajulikane tu kwa wanandoa-wenzao.

Mfano, wapo ndugu zetu unamwona kavaa nguo za kiume lakini katika sehemu zake za siri ni mwanamke (au anazo sehemu za siri zote mbili).

Ya mwisho kwa upande wangu na jinsi nilivyosoma: uoga wote ule wakufichua "siri" ya sehemu hizo ni moja tu ya malezi, sawasawa tu na uoga wamngurumo, uoga wa nyoka na kadhalika. Lakini nimesikia yapo makabila mengi duniani kotekote yasiyokuwa na mambo hayo ya kujifichaficha hovyo.

katawa said...

Lazima ziendelee kuwa sehmu za siri kwa kuwa kila mtu anayo dizaini yake anayopenda aijue yeye na mwanandoa mwenzake.

Sehemu zingine za siri ni nyeusi tii,zingine kubwa ,ndogo nyeupe na wengine hawana hizo sehemu za siri

Nakushauri endelea kuzifanya ziwe sehem za siri

emu-three said...

Hapo ni lugha tu, ...`sehemu za siri'...lakini labda tungeziita `sehemu za aibu' kwasababu ukitizamwa neti zako ni `aibu' sehemu hizo ni kwa ajili yako kutizama na mwandani wako...sijui wala wanatembea na huyu au yule kwali zinaweza kuwa sehemu za aibu?

emu-three said...

Hapo ni lugha tu, ...`sehemu za siri'...lakini labda tungeziita `sehemu za aibu' kwasababu ukitizamwa neti zako ni `aibu' sehemu hizo ni kwa ajili yako kutizama na mwandani wako...sijui wala wanatembea na huyu au yule kwali zinaweza kuwa sehemu za aibu?
Lakini kwa watu wa imani, mwenyezimungu katuagiza kuwa `tujisitiri' sehemu hizo nyeti Qur'an 33:59