Tuesday, March 8, 2011

kama tungemuabudu Mungu mama........

eti ni siku ya wanawake duniani, ya kujimwaga, siku moja tu kwa kila mwaka! wakati kila siku twahudumiwa na wanawake

nafurahia uwepo wa wmanamke, mwanamke akila chakukla alia jamii nzima, akinywa maji anywea jamii nzima. nilimjua mzazi wangu wa kike nikiwa na miaka kama 20 hivi na hivyo sikuenjoy, nimepata suruba nyingi kutoka kwa wanawake kadhaa japo ni wachache lakini wapo

upendo wa mwanamke ni ule wa kweli, hauna wivu wala kihehere here, najiona mtoto mdogo mbele ya mzazi mwenzangu! naushangaa upendo wake, jinsi anavyotutunza, kutulea na hata kututomasatosa mimi na mtoto mwenzangu kwake

kama dini zetu hizi zingemuabudu Mungu mama, tusingekuwa na vita wala migogoro ya kidini kwani Mama hana wivu uliopitiliza, halipizi kisasi na ni mwingi wa kusamehe tofauti na baba.

sijui kama vitabu vya dini vingeandikwa na wanawake vingevutia kiasi gani!

great is a woman

3 comments:

emu-three said...

Mkuu unasema `mungu mama?' Unanikumbusha enzi za Wagiriki, Wayunani, na nai vile, walikuwa na miungu wengi, wapo miungu wa mapenzi, miungu nani na nani...
Ni kweli akina mama ndio wanaojua nini maana ya kupenda, kuvumiliana nk, kwao wao `amani; ni tunu. Wengi wanaishia kumwaga damu au kuanzisha chochoko za kumwaga damu ni wanaume, lakini waathirika wakubwa ni wanawake na watoto.
Ugomvi aanzishe mwingine, kuumia waumie wanawake na watoto!

Yasinta Ngonyani said...

Kwanza napenda kusema Ahsante nikiwa kama mwanamke. Na napenda kuwapa Hongera wanawake wote duniani. Upendo Daima. Inabidi wanawake tusimame imara na Kumbuka kwamba wanawake ni nguzo ya taifa na pia tukijishughusha tunaweza.

katawa said...

Kwa jina la MAMA na la BINTI na ROHO mtakatifu.Amen