Tuesday, March 1, 2011

Kikwete na hofu ya vurugu za chadema

Angalizo: sipendi kuongelea mambo ya kisiasa hata kidogo, kwa hili nimelazimika

Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi raisi Kikwete aliongelea juu ya kile alichokiita vurugu za maandamano ya chadema ya kuvuruga nchi kwamba ugumu wa maisha ndilo serikali yake inaoushughulikia.

Sioni haja ya lawama, naamini ni rahisi sana kuiedeza Tanzania kwa kubadilisha mifumo ya kiutawala

Kwanini kikwete asiwaite wanaolalamika na kajadiliana nao juu ya nini kifanyike ili nchi iendelee ili mambo yabadilike? Zile anazoziita vurugu zinatokana na ugumu wa maisha na sio chadema

Maandamano yanayoendelea kwenye nchi za kiarabu ya kuzipinga serikali zao kwa wingi hayatokani na wanasiasa wala wapinzani bali ni wanaharakati wanaokutana na hali ngumu na ugumu wa maisha. Viongozi wa serikali hawaoni ugumu wa maisha, wanaona mambo mswano kwa kuwa wao wako vizuri, hii inakamiisha msemo wa kihaya usemao kuwa aliyeshiba haoni uchungu alionao mwenye njaa

Badala ya kurekebisha mambo serikali na wanasiasa wako bize kurekebisha maisha yao, kujiongezea malipo, kununua magari ya kifahali na ya kisasa huku wananchi walio wengi wanalia na kusaga meno

Ni mwambie tu kikwete kwamba historia ya vurugu zinazoendelea nchi za kiarabu hazitokani na wanasisa bali ni wananchi wenyewe, hata Chadema wakikaa kimya, wananchi wenyewe wataibuka na kulipuka wenyewe

Tunahitaji mjadala wa kitaifa na kurekebisha mambo na sio kuwalalamikia wale wanaohamasisha wananchi, tena Chadema wanasaidia kuelekeza zile hasira ziende kwa utaratibu na sio kulipuka zikatuingiza matatani kama watanzania.

Viongozi wetu washuke chini na kujua hali halisi na sio kuwalalamikia wapinzani. Naamini Kikwete ana uzoefu wa kutosha kuongoza nchi, na autumie uzoefu huo kubadilisha hii hali, kumbuka tulihaidiwa maisha bora kwa kila mtanzaniia na kwenye ubora basi hamna vurugu wala maandamano. Litekelezwe hilo

No comments: