Monday, March 28, 2011

kile tukiombacho

katika sara au maombi watu humpayukia Mungu wakidhani wanaomba vitu muhimu, Mungu huonekana kutokuwajaalia vitu hivyo na kuwafanya kulalamika. kumbe wanaepushwa na matatizo makubwa.

kuna wakati mvua hukosekana (ila sijawahi sikia kukosekana kwa jua) na watu huomba, mvua huja na kuleta mafuriko ya hatari kuliko jua (bora wasingeliomba hilo)

kuna wanaoomba panya waondoke ndani/nyumbani, labda bila kujua kwanini Mungu kawajaalia panya, na ili panya waondoke kwa njia ya maombi, basi nyoka huingia nyumbani! wanaona panya kimya, wakigundua kuna nyoka, basi huomba aondoke na wakisikia panya karudi wanamshukuru Mungu kuwa hii ni ishara ya kutokuwepo nyoka!

1 comment:

emu-three said...

Hahaha, mkuu wazo lako la leo ...mmh!