Monday, March 14, 2011

matibabu Loliondo, unataka kupona ili iweje?

watu wanamiminika kwa yule mzee au babu wa Loliondo kupata matibabu. muujiza ni kwamba kuna wagonjwa waliotoroka hospitalini kwenda kule na walipofika wakajikuta wako foleni moja na madaktari wao! hata anayetibu wagonjwa ni mgonjwa asiyeweza kutibika hospotalini kwake!

ila sasa yawezekana kweliyule mzee katumwa na Mungu na niseme kwamba kiimani mambo yote yanawezekana na tusijiulize kwanini huyo Mungu amuagize yule mzee tena Loliondo na sio kijijini kwenu

watu wanapenda kuponywa japo hawako tayari kujiponya! ujiulize swali, unataka kupona ili iweje? upone ukimwi ili ufanye ngono sana? upone kisukari ili ule sana au

lakini ni kweli kwamba mungu anaponya kupitia kwa yule babu pekee? hivi sisi hatuwezi kuongea na Mungu?

magonjwa yoote yasumbuayo huwa yanatokana na ulaji wa hovyo. nimefikia hatua nimeachana na biashara ya kufundisha utambuzi. huweleweki na unaonekana chizi, hamna wafuasi wa kanuni za ulaji bora

ukiwaambia watu wasile hovyo wanakuona mjinga na eti hau-enjoy maisha. sasa hao wanafukuzana loliondo kutokana na ku-enjoy vyakula vya hovyo.

unaona kiongozi wa serikali dini na watu wengine wanavitambi, wanakula hovyo harafu eti wanaenda loliondo. tunapenda kutibu dalili kuliko mizizi

sijui kama kuna anayefuatailia kanuni bora za chakula atakayeenda loliondo iwe inaponya au la!

na Mungu wa mzee yule hataki watu wafe! kanun ya kuuvua mwili iliwekwa kimakosa??

lakini kwanini woote tutake kupona?

4 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Dah! inahitaji kichwa cha mwendawazimu uweze kueleweka...

Anonymous said...

Umenena sawa Kamala, ngoja nimwambie Maggid alink hii kwenye blogu yake tupate comments za watu! lol you made my day!

Anonymous said...

Kila mtu anapenda kubaki na mwili wake wa nyama kwani huo ndiyo unaohitajika sana kwenye ulimwengu huu! Ukiangalia sana kila kitu kinachotengezwa na binadamu ni kwa ajili ya mwili huo huo. Lakini kama ulivyosema kuhusu kujitibu ni somo gumu sana! Mzee kanyama na mapocho pocho mengine kazi sana kuacha inataka moyo. Nikija kwa swali lako nataka nipone niendelee jufaidi maisha!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

anony kufaidi maisha?? tunafaidije maisha? kwanini basi tusiishi ili tusiugue badala ya kujiachia tukaugua na kutufuta misaada ya ndoto za kimungu? je tunaishi ili tule au tunakula ili tuishi?

faida ya maisha ni ipi hiyo?