Wednesday, March 30, 2011

matusi, unatukanika wewe?


kuna vitu vinaitwa matusi na kutukanana, ufikia pahala pa watu kutokuongea pamoja, ungomvi nk. kisa?? eti jamaa kamtukana! aghh

matusi kama pumbavu, mjinga, fala lione nk, huleta ugomvi. lakini mtu akisema tusi hilo unakuwa hivyo?

matusi kama mbwa wee, paka, tako nk, hivi mtu akikwambia hivyo unakuwa hivyo kweli? kwanini sasa umchukie wakati anauhuru wa kuelezea kile akifikiriapo juu yako?

3 comments:

chib said...

Ni hulka ya binadamu, nafikiri mtu akituswi kama ana takao kama la malaika, atakasirika tu, japo tunaimani malaika ni mzuri tuuu.
Wakti mwingine wala hata sio tusi, kwani mtu akikuambia kinyeo chako wee, amekutukana au amekisema tu. Sasa hasira za nini?

SIMON KITURURU said...

Binadamu utamuweza!Mambo zake valuvalu yani!:-(

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

“The first human who hurled an insult instead of a stone was the founder of civilization.” Sigmund Freud