Wednesday, March 23, 2011

mkoa kagera na mvua, utelezi!

ni msimu mtamu sana kwa wakulima, nimezunguka wilaya zote za mkoa kagera, mvua zilikuwa ni kama zimegoma, kumbe zilichelewa kidogo, sasa zinatema, ni baridi na ni balaa. sasa mazao yanachekelea shambani, yanakua kwa furaha, ni matamu kuanngalia

japo watu wa hali ya hewa wanaai hamna mvua, mvua zilizokwishanyesha hapa hata zikikoma mazao yatastawi tu japo bei za chakula zinapanda tu

sasa kabla ya kuoga huwa kwanza nakimbia kimbia ili nichangamshe viungo, niko mlango wa nyuma wa nyumbani kwetu (labda kwangu), kuna utelezi, nilikuwa nimebeba ndoo ya taka taka nikitokea nje, kifua wazi, natelez, purrrrrrrrrrrrrrrr mpaka chini

nilicheka kwanza, japo sikuumia sana, nikavuta kumbu kumbu mara ya mwisho niliteleza na kudondoka mwaka jana nikiwa Dar pale ferry

inachekesha kama sio kufurahisha kuona jitu zima kama mimi linateleza na kudondoka chini pwaaa

1 comment:

danie said...

pole kiongozi haya ndo maisha ila kama vile ulikuwa na kaudhembe fulan in maana ukuona kama ni hatari hapo?
na vipi ulikuwa hujambeba baby