Thursday, March 10, 2011

tatizo la TZ sio CHADEMA, ni hali duni

wanasiasa wanakilauma chama cha CHADEMA kwamba kinaleta fujo, oh kinataka kuipindua serikali. lakini uhalisia tatizo sio CHADEMA bali na hali halisi ya mambo. tena bora CHADEMA kinashikila na kukongozi bomu la hasira ili lisilipuke vibaya

wakiongelea bei ya vyakula, wanalaumu mvua kutokunyesha, interesting. vijiji vingi vimezungukwa na mito vijito na maziwa, tunasubilia mvua? kuna sehemu ambazo kusambaza maji haigharimu hata milioni hamsini, lakini tunasubilia mvua na serikali inasingizia mvua badala ya kusambaza maji kifanyike kilimo cha umwagiliaji, haina pesa za kusambaza maji lakini ina pesa za mashangingi ya milioni miambili

eti mafuta yamepanda duniani kote, ni sawa, lakini mbonamataifa mengine yana uhafadhali?

CHADEMA inalalamikia wizi wa kura za majimbo kadhaa, kama serikali ingetenda kazi yake na kuwaridhisha wananchi, CHADEMA isingekuwa na wafuasi kwenye maandamano na mikutano yake

bora serikali itumie rasilimali zilizopo kurekebisha hali ngumu ya maisha vinginevyo tatizo sio chadema kwani hata kama chadema ikifa, fukoto litafukuta tena vibaya.
ni mtizamo

3 comments:

chib said...

CCM haina mvuto tena!

emu-three said...

Tatizo mbu wanamkera jamaa akinywa mvinyo kwenye kiti kirefu!

John Mwaipopo said...

tawire waitu