Monday, April 4, 2011

heshima, nidhamu

najuliza heshima na nidhamu ni kitu gani, watu wengi hudai heshima na nidhamu kutoka kwa wengine, je heshima na nidhamu ni kitu gani? tulipokuwa wadogo tulilelewa kigaidi, tulipigwa na yeyeto kisa katuzidi umri na kwa mtizamo wake hatuna nidhamu. jamii hii ilikuwa ya ajabu. binafisi nilikwidwa sana kwa visingizio kwa kutokuwa na heshima, nina hasira nao mpaka leo hiv nani anayejua kuwa fulani hana heshima je wale wapuuzi wa zamani waliotukwida waweza kutukwida leo au kuwakwida wadogo kisa heshima? si tutaandamana na kuwapiga mawe kama sio kuwapindua?

4 comments:

emu-three said...

Nidhamu na heshima ina tafsiri ile ile, nia ni `adabu njema'. Ndio wengine wanafikiri kuchapa sana, au kupiga kunamjenga mtu awe na nidhamu...inawezekana ikawa hivyo lakini ni `nidhamu ya woga'
Lakini hata hivyo wakati mwingine mtoto anaweza asisikie kabisa bila kuchapwa kidogo...wengine tunayakumbuka hayo kwa wema, kuwa kama mzee asingenichapa kwa kosa lile, leo ningekuwa `mtukutu'...ila sio kuumiza!

Goodman Manyanya Phiri said...

Heshima na nidhamu vinao msingi moja. Nao ni kutenda kile kinachotarajiwa kwako ikiwa wewe ni mstaarabu. Na ukifanya mara kwa mara kinyume na matarajio hayo ya jamii yako, basi wewe "hunanidhamu, huna heshima, pia wewe siye mstaarabu au mchapakazi"


Kitakachokukuna ki mawazo ni kwamba, jamii ikiharibika, kwa mfano, kukiwa na vita, hasa vita ya wenyewe kwa wenyewe, wale wote waliokuwa wanatazamwa kama ni watu wasiyekuwa na heshima wala nidhamu ndio wanaibuka kama mashujaa!!!!

Lamwisho, Mkuu, kwa upande wangu. Nidhamu na heshima, kama ninavyoelewa kisayansi, mtu hurithi sawasawa tu unavyorithi urefu, ufupi, rangi ya ngozi na kadhalika. Pili nidhamu na heshima unaongeza jinsi unavyochunga unakula nini.."GOD IS IN THE MOLECULE"!

Anonymous said...

kamala kama usingechapwa,ninavyo kuona wewe leo hii ungekuwa unatukana matusi ya nguoni mpaka kwenye blogu.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

unauhakika sasa situkani??