Tuesday, April 26, 2011

mpaka lini nitapongezwa kwa sikukuu?

kwangu siku zote nikubwa tu. wakatoliki wana ijumaa kuu ya kutokula nyama, mimi siku zote kamwe sili nyama wala viumbe hai, kwahi basi kila siku ni ijumaa kuu

saimini sana historia, kwa hata tafsiri yangu juu ya Yesu, mkate (ekaristi) naviangalia kwa tafsiri kubwa zaidi

kwa ufupi, kila siku kwangu nikuu, ni kubwa kwa sababu kila siku ninauhai, naishi kimungu na maisha yanaendelea. kwa nini kupongezwa kwa tarehe ya kidini eti nikuu?

siku zote kwangu ni kubwa sio pasaka krimass, birthday wala siku ya ndoa

labda pongezi za sikukuu kwangu zipungue wewe unaonaje??

labda nikupongeze basi kwa sikukuu kwako.

heri ya pasaka muumini

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa Pongezi ...ila wewe kwa matata nakuamini:-)

Goodman Manyanya Phiri said...

Unanitia wasiwasi Kamala. Unakuwa kama mtu asiekanyaga ndani ya jengo la kanisa.


Hata hapo utakuwa hukosei kwani tunaambiwa "jengo la kanisa" (TEMPLE) ni mwili wamtu wala si matofari.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@manyanya hilo ndilo ninaloliamini zaidi na kulitukuza na sio yale mengine. hata nikienda sio kwa kitu chochote zaidi ya kubadili mazinngira kuimba kidogo nk

Anonymous said...

huo kamala mimi ndio naita upumbavu si uliona jamaa alivyo mpiga kibao mzee wa watu eti kwani watu fulani tunasherehekea hiyo siku kuu kwa pamoja!!!!!!???????