Wednesday, April 20, 2011

nani anaratibu maadili ya wazee?

kila kona ukipita utakutana na wazee wakilalamika ya kuwa vijana wa siku hizi ni hovyo kabisa na hawana maadili, najiuliza maadili nini na ninani anayeyaweka maadili na kuamua yawe maadili then yafae kufuatwa na kila mmoja na vizazi vyote.

wazee wengi wanalalamika ya kuwa vijana hawana maadili, nawaangalia nashindwa kuwaelewa, labda wana wivu kwa maisha na miendendo ya vijana. eti vijana hawana maadili, hivi ni nani mwenye kuratibu kujua kuwa wazee hawana maadili na wala hawafuati maadili? je ni kweli sasa wazee wenywe wanafuata maadili?

si mnajua mifumo yote huwekwa na wazee kwa manufaa yao? soma biblia uone, amri na makatazo mengi yanalinda maslahi ya wazee, mf waheshimu baba yako na mama yako siku zako zipate kuwa nyingi nk hamnaga waheshim watoto wako au wadogo wako, je kwa kutokuwaheshimu wadogo wazee wanakuwa na maadili kweli? nani anayewaratibu?

nami nasema, kila mzee anayemlalamikia kijana basi hana maadili!

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hapo sasa! kaaazi kwelikweli...!!

Mcharia said...

Wewe kamala!!

SIMON KITURURU said...

Duh!

Goodman Manyanya Phiri said...

Wazee wanao wajibu wa kuwalea vijana. Wajibu siyo kuwahukumu vijana kwani popote pale waliposhindwa watoto ni ishara ya kushindwa kwao wazee wenyewe katika malezi.

Lakini usiseme haraka, Kamala, kwani nawe hivi karibuni utaanza kuwakosowa vijana!

Nimependa lakini ulipopendekeza [wazee nao hawana budi kuwaheshimu vijana].

Hiyo ni ukweli kabisa kisaikolojia ("mtoto ni 'mtu mzima mdogo'").


Hata kifalsafa pendekezo lako Kamala nipendekezo murwa kabisa("kama wote lazima wapitie utoto lakini kutokana na kifo sio wote wanaofikia uzee, basi 'utoto ndiyo ukongwe'").

Hayo kama sikosei ni mawazo ya akina Socrates na Plato miaka zaidi 2000 iliepita huko Ugriki ya zamani.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

"kila mzee anayemlalamikia kijana basi hana maadili!"

Nimependa hitimisho lako ingawa sina uhakika kama (lote) limetokana na hoja ulizozitoa.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@manyanya, sitowakosoa kabisa, sina mpango huo