Wednesday, April 27, 2011

tiba ya babu na 'karma', upone ili iweje?

suala hapa sio hofu ya kama dawa ya babu inaponya au haiponyi, inafuatana na kiwango chako cha imani kikoje kwani imani ina nguvu sana. mimi siwezi kwenda kwa babu, nina kila uponyaji na jinsi ya kuufikia. ninaye babu yangu wa kunilinda na namhishi, labda tumuite master au Mungu ambaye wengi hudhani twamishi

ila sasa, ukiangalia watu wanavyomiminika loliondo kupona! labda nisema kuwa wengi tunaugua karma, magonjwa mengi yanatokana na matendo tuyatendayo maumivu tuwapayo wengine na kula hovyo vyakula vya gharama lakini ni sumu, kutokujua utaratibu wa kula nk

jiulize kama babu anaponya kweli nawe unaenda kupona, je kama wewe ni mchawi, unataka kuponywa na Mungu ili uzidi kuwaroga watu wa Mungu? unataka kuponywa na Mungu ili uzidi kuwaibia watu wa Mungu? unataka kuponywa ili uzidi kuwazinisha watu wa Mungu? unataka kupona ili uzidi kuuwa viumbe vya Mungu?

maisha ninini mpaka uyag'ang'anie lakini je kifo ni nini pia? kuna kitu kinaitwa karma. hapa ndo kuna chanzo cha maumivu yetu. kila tuliwazalo, tulitendalo na tulisemayo huwa tunatengeneza nguvu na nguvu hiyo huturudia, bahati mbaya sisi twatengeneza nguvu hasi zaidi ya kuwaumiza wengine kuliko chanya, nguvu hii huturudia

hata babu akituponya tutaugua tu kwani sisi hataponyi matendo yetu, tunataka kupona ili tuendelee kuwaumiza wengine, mwishowe twaumia na sisi kukliko tuwaumizavyo wengine

1 comment:

Anonymous said...

nawapendaga watu wa saikolijia lakini sehemu nyingine huwa mnajinga wenyewe sasa wewe kamara unaogopa kula nyama ili iweje ilikusudi uishi maisha marefu eeeeeeeeeeeeeeee!!!!!???mwalimu wako munga naye alikuwa anasema hali nyama ataishi muda murefu hatakufa mapema sasa sijui mapema yake ilikua lini wakati mwingine mnajichanganya wenyewe