Monday, April 11, 2011

ulevi na usumbufu!

kwa muda mrfu naishi na jiranimlevi. mzee huyu na mkewe watu wenye umri mkubwa hunywa pombe, hulewa na kuja kutufungulia muziki kwa sauti ya juu.

naishi eneo la misheni ambako pombe ni mwiko. sasa nashindwa kujua ni kwa nini tabia yake hii inafumbiwa macho. kuna wakati nilimpiga mkwara akawa mpole na kuniona kama kituo cha polisi

sasa jana usiku ikawa noma, mkewe anakuja nyumbani kwangu na kuanza kumrushia mkewangu maneno, mke wangu ambaya hanaga ubaya na mtu.

nikawafata kwao nakuwafunda, wakaleta ubabe, nikawaonya kuwa naweza kuvua tamaduni za mkubwa huheshimiwa na kuwashushia kipigo kikali, nikaangalia nguvu nilizonazo nikimtwanga mzee kama yule kofi au ngumi ni mpaka mochwari.

jioni hii naenda kumfunda na kumwonya vinginevyo atanitambua.

yaani nafikia hutua ya kuuvua utambuzi uzuiao ugomvi na hasira ili heshima irudi au sio wakuu?

1 comment:

freddy mbeyella said...

Kamala, kuwa na utambuzi haimanishi kuwa malaika! Nadhani ukijitambua inakuasaidia kupunguza maumivu kwenye matukio ambayo kwa mazoea tunayaita mabaya. Ebu jikague inawezekana wewe ndiye mlevi!"tafsiri zako" kama si hivyo kuwa wewe na muache mzee awe yeye! Najua unaweza sana!