Saturday, April 30, 2011

wafanya kazi wa maabara, huwa naona aibu

magonjwa ya tumbo ni kama sehemu ya maisha. bila kujali wala nini. tusiokula nyama (vegeterians) huwa tuna ka-risk kakuugua magonjwa ya tumbo. hii i kutokana na mamzingizra ya kutengenezea chakula kama sio makini basi ni ishu

ila sasa, uendapo hosp unasumbuliwa na tumbo, huwa unaambiwa ukanye kidogo na kumletea mtaalamu wa kuangalia kinyesi a.k.a mavi. basi wanya, wachokunoa na kuchagua kipande, then wamletea!! huwa naona soo. wagonjwa wenzio mnapishana koridoni wanaangalia ulivyobebelea utadhania ugali, kumbe msosi ulokula jana!! ahhh

kuna jamaa yangu alipokuwa mdogo alielekezwa, akapewa likopo likubwa, jamaa aliweka kipande kizima ua kinyesi.jamaa wa maabara alishangaa

ila sasa, wafanyakazi wa maabara ndo huwa sielewi. wao kazi yao ni kuangalia mikoja, vinyesi, damu na kutoboa miili ya watu, huwa sielewi hapo! labda wamezoea.

ni sawa na mwanamke kukutana na dokta wakiume aliyemzalisha, si unajua amjua vizuri sana

ila kazi ya kupima vinyesi ndo kali kuliko zote. nikikutana najamaa waangalia kinysi changu duh huwa nakumbuka mengi na kujiuliza mengi pia. kazi ni kazi lakini

3 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

kamala mgonjwa kweli jamaani!


naona wataendelea tu kumtoa vitu zaidi huko maabara!

Mcharia said...

Naona unahitaji tiba

SIMON KITURURU said...

Hahahahaha ! Komandoo Kamala hujatulia unajua!:-)