Monday, May 9, 2011

bwana Yesu Asifiwe: kwalipi?

kuna badhi ya vitu tukiambiwa tunatarajiwa kuitikia vile yule aliyetwambia anategemea/anahitaji/anatarajia tumjibu.

nilipokuwa mwanafunzi na mkristo mzoefu nilikuwa karibu na jamaa mmoja aliyekuwa anasomea uchungaji. basi njaa inauma, ni muda wa kula, anasimama jamaa na kusema "bwana yesu asifiwe", yule jamaa yangu anayesomea uchungaji akajibu, "kwalipi?"

nikasutuka, nikashangaa na kujiuliza kumbu kuna majibu mbadala na sio lazima AMEN?

basi kwenye nyumba za ibada mtu akisema haleluya, mnajibu Amen! hamnaga jibu mbadala

najiuliza, mtu akibisha Hodi nyumbani kwako na hutaki aingie ndani, unajibuje? si ni lazima useme karibu?

tunahitaji kuwa na majibu /misamiati mbadala vinginevyo hatuko huru.

shikamoo... kama hutaki kuipokea hiyo shikamoo unajibuje? shikamoo mwenyewe

2 comments:

SIMON KITURURU said...

Tatizo sidhani ni maneno kutokuwepo! Nafikiri jamii yetu ni ya woga !

Ni watu wa kukubalikubali bila kujiuliza!

Nafikiri Jamii yetu ingekuwa ni ya kujiuliza !Salamu kama Shikamoo tusingekuwa nayo!

Lakini huu naamini wakati wa mpito!

Baadaye sio tu Bwana asifiwe watu watajiuliza ni kwanini waitikie AMEN,...
... bali mpaka mtu akiitwa MHESHIMIWA watachunguza kama kweli anastahili kuitwa Mheshimiwa!

Goodman Manyanya Phiri said...

Mkuu, misemo kama hiyo ni kama "vyombo" au TEMPLATES tu vya mawasiliano; sio lazima uyaingilie ndani yake zaidi lasivyo unaweza kuumia kichwa bure.


Si unaukumbuka ule mchoro wa mtu mwenye nywele, meno na macho vya kutisha akiwa amesimama na mtu wastani asietisha? Chini ya mchoro waliandika:


"DON'T ARGUE WITH A FOOL! PEOPLE MAY NOT NOTICE THE DIFFERENCE!"


Kama hutaki mtu aingie nyumbani mwako kwa ile "hodi" yake, NYAMAZA TU!!!


Mimi binafsi simwamini Yesu wala Mohammed hata kidogo (labda baadaye nitakuwa Myahudi kidini kwani naamini Kristu hajawahi kufika bado) lakini Mkrestu akisema "Asifiwe" naitika kama inavyostahili: "Amen!".


Akija Muislam kwangu na mambo ya dini yake naye nampa heshima inavyostahili.


Tukianza kuulizana mantiki zote katika dini zetu (pia na desturi) mbona dunia itakuwa ndogo kwetu sote!


Napenda Wazungu wanaposema: "JUST LIVE AND LET LIVE!"