Thursday, May 26, 2011

ipo siku nitampiga picha trafiiki akipokea rushwa!

nikiwa natokea nyumbani ninakoiishi mwendo wa kama km10 hivi nje ya mji wa bukoba na kuwahi usafiri, nilichukua pikipiki ya kukodi. njiani twakutana na askari polisi, wasimamisha pikipiki na kumkuta dereva wangu akiwa na lesseni ya gari badala ya ile ya pikipiki.

wakaniamuru nishuke, kisa pikipiki imekamatwa. duh kali hii, nawaambia mimi nawahi basi mnanishusha sina makosa, kwanini msimruhusu anifikishe then aende kituoni?

wakanibishia na kusema nimewatukana na kwa ubabe wakachomoa swich ya pikipiki na kusema shauri yako, jifanye mjanja unayejua kutukana.

sikuwa na jinsi, nikawashauri watumie akili na utu kidogo then nikatembea kwa mguu kuwahi safari yangu. nafika mbele kidogo naona mmoja wa madereva pikipiki, namaaskri wakatpita mbio. nikamuuliza vp? akaniambia washachukua rushwa sasa waondoka hao!

sasa nitaitumia kamera yangu vizuri, nitawapiga picha wakichukua fedha haramu kama kumbukumbu na kuzipeleka kwenye vyombo vya habari nione kama kuna hatua zitachukuliwa. jamaa wanaangalia pesa tuu na kufikiri mafanikio yetu yapo kwenye fedha hata kama sio halali au zaacha watu wakilalamika!

2 comments:

SIMON KITURURU said...

Rushwa tamu!
Na kwa bahati mbaya haiko kipesa tu hasa nasikia kuwa kuna mpaka rushwa za ngono kuanzia majumbani kwa mke na mume mpka makazini ambago ikitolewa ni mrembo atakayepandishwa cheo na bosi!

emu-three said...

Rushwa kajaa tele kila kona,usiombe uwe na mgonjwa ukamfikisha hospitali zetu hizi, ndio unakuta umati wa watu...utafanyaje, dawa ni kumuita chonjo nesi aweke cheti chako juu...hii inaitwa nini?
Haya unataka umeme, umeshaweka line, kila kitu imebakia nini, kuingiza mwanga ndani, ukifika Taa la Neskori, wanakuambia zamu yako bado, wakati umeshanunua runinga na nyumba mbeho...dawa ni nini...mtafute mtu anayeitwa kishoka, mtaongea naye mtakubaliana, naye anaenda kuongea na wanaohusika, unaambiwa utoe hela ya taxi , kwani mgari hakuna...hiyo inaitwa nini...
Mungu wangu, natafuta kazi nimehangaika wee, nikakutana na jamaa yangu akaniambia ukitaka kazi ufanye kazi, akaichukua barua yangu na kwenda kuongea na meneja uajiri...duh, nikawa miongoni mwa wa ku---fanyiwa nini vile, na hata hiyo kuhojiwa kwenyewe hakukufanyika...kazi ikajileta! Hiyo inaitwa nini....
Oh, Rushwa bwana ni rafiki wa kila mtu, anauma ukimtoa, lakini mtamu ukimpokea!