Tuesday, May 24, 2011

Jamii yetu inatufunga minyororo na kutuburuza jela za hiari

kwa miaka kadhaa tangu nijitambue nimejitenga na mifumo mingi ya jamii. huwa siendagi sana harusini na kuhudhuria na misiba.
baada ya migogoro isiyoisha na kutafutana, nimeamua kujitenga na familia niliyotokea kwa kiasi kikubwa na kuishi kivyangu.

ila sasa kila nikienda katika jamii ni mikwara na vfungo. watu wanafanya harusi kumbe wanatafutana ili kuona huyu kaleta nini, ana nini na kaja nanini. misibani hivyo hivyo. baada ya shughuli hizi huwa ni masengenyo na majigambo yasiyoisha. kumbe jamii yetu ni minyororona gereza tusizoweza kujitoa.

tunafanya harusi kubwa then tunabakia na maumivu ya mmadeni na nguvu nk,, kwanini tusiache.
hamna kusameheana wala kuchukuliana bali kuhukumiana.

sisi kama jamii tunakifungo kikali kuliko cha wale jamaa walioko jera.

1 comment:

Goodman Manyanya Phiri said...

Hilo ni neno kweli!

Mimi napenda msemo waKizungu:


A FOOL AND HIS MONEY EASILY PART

(Yaani: "Wale wanaopenda kujionyesha utajiri ndio wajinga wa kupindukia")

Utakuta wanafanya msiba wenye hela kubwa (sanduku tu: Shilingi Bilioni) wakati wanao ndugu zao wa damu wanaolala kwa njaa!


Tena sanduku lenyewe wajanja watakuja kuchimba usiku waibe na kumdondosha maiti aje kuigusa ile sehemu inaostahili: UDONGO WA MWENYEZI MUNGU!