Saturday, May 14, 2011

kikwete anaujasiri gani wa kuhudhuria uapishwaji wa Museveni?

maraisi wa Afrika uwa siwaelewi hata kidogo akili zao na maamuzi yao. sasa rais wa Tanzania Jakaya kikwete alihudhuria kuapishwa kwa rais Museveni wa Uganda

sielewi ni kwa ujasiri gani kikwete anahudhuria sherehe hizo. Museveni kwakutumia vyombo vyake vya uhasama (wao wanaita vyombo va usalama) anauwa na kunyanyasa watu wake hivi hivi. Tanzania kama nchi jiarani, Jumuiya ya Afrika mashariki ambayo tanzania ni member na makao yake makuu yako Tanzania ziko kimya utafikiri Museveni anawakomboa watu wake.

lakini likija suala la kuapishwa tena kuwa rais, eti hao wanaona umuhimu. hivi viongozi wetu ni wetu na ni wenzetu au wanamambo yao binafsi kupitia sisi? inakuwaje maraisi kibao wanaenda kubariki uapisho wa mtu anayeuwa na kunyanyasa watu bila hatia harafa wanashangilia utafikiri yanafanyika mambo ya maana na ya msingi kumbe ni kuua watu tu?

kwa nini hawana tamko lolote na badala yake wanakimbilia sherehe uchwara? kwanini kikwete kama rais jirani hawezi kukemea?

wanaona waganda ni mizigo tu na sio watu isipokuwa rais kigang'anizi kama Museveni? ndio maana wazungu wanaisurubu libya huku viongozi wa afrika wako kimya

ndio maana watanzania wanaishi maisha ya shida huku kikwete na serikali yake vikikubatia uwekezaji wa kinyama na kudai eti uchumi wetu unakua, kwa ajili ya nani?

anyway sipendelei mambo ya kisiasa lakini kwa mauaji anayoedesha Museveni, kikwete kama rais wa taifa la wetu wenye utu alipaswa kukemea mauaji na manyanyaso kiliko kukimbielia uapishwaji.

Mungu wa wanasiasa naye simuelewi, eti wanaapa eeh Mungu nisaidie. kwa hili kikwete kadhiirisha kuwa uongozi wetu uko kinyume wa wananchi kwani angesimama upande wa wananchi wa uganda kama raia wa Jumuiya ya Afrika mashariki na jirani na binadamu wenzetu na sio upande wa rais muuaji.

vinginevyo na sisi Tanzania ipo siku tutaingia mitaani kwa ukali wa maisha tuone kama watashirikiana kutumaliza

3 comments:

chib said...

Labda ameanza kuona kuna moto unataka kuwaka Bongo, kwa hiyo anenda kupata maarifa au kuandaa makazi ya kukimbilia moto ukipamba moto!

SIMON KITURURU said...

Mmmmmhhh!

Mbele said...

Alipoingia urais katika awamu ya kwanza, nilimpigia debe JK, kama walivyofanya wengine. Tena nilifanya hivyo kwa maandishi, ikiwemo katika kitabu cha CHANGAMOTO.

Hali ikabadilika. Ninapojiuliza kwa nini JK aligombea awamu ya pili, napata picha kuwa alifanya hivyo ili kuulinda ufisadi, ambao ni mtaji wa CCM.