Wednesday, May 18, 2011

malaria inakubalika!!

sio kwamba nampinga yeyeyote, ila kunamaneno kibao ya kutokubalikwa kwa malaria hapa nchini. mwenzenu sasa niko hao kwa siku ya tatu leo. kidume na nguvu zangu zote nimelala dwii, siamki nahudumiwa kitandani. ni malaria.

takwimu zinaonyesha wazi kuwa mkoa kagera unaongoza kwa maambukizi ya maralia bilia shaka na mbu waenezao malaria ukifuatiwa na Mara. sasa nakutana na songombingo.

serikali inasambaza vyandurua vyenye dawa! ili kutukinga. nimepata chandarua hiki kwa shs 500 mwaka jana na kingine mwaka huu. huwa napulizia dawa kila siku lakini du bao malaria niyangu. sijui nifanye nini ili kumlinda mrithi wangu dhidi ya gonjwa hili. ni changamoto

na kwa kuwa sijaugua gonjwa hili kwa miaka kama mitatu sasa, nimejifunza kuwa huu ni ugonjwa hatari sana. waweza kuwa kichaa au hata kufa kiaina.

natumia dawa za mitishamba tu kwani naamini ndizo dawa pekee zenye kuweza kukabiliana na ugonjwa huu kwa ufanisi bila kuwa na side-effects.

kupona nilazima kwani bado nipo

3 comments:

SIMON KITURURU said...

Kwa bahati mbaya sijasikia kama kikombe cha babu kinatibu mpaka Malaria bado ,...
... ningeshauri umcheki!Tukiacha utani:

Ugua pole Kamanda! Na pole sana kwa hii kitu! Mie ilinilaza muda kibao safari yangu ya juzijuzi Morogoro mpaka sikuonekana mahala kibao nilikotegemea kuonekana!

chib said...

Ugua pole Kamala, tukiona kimya muda mrefu tutaitisha hitma!

Ujue, dawa karibu zote zinatokana na mitishamba, ila zimebambikwa majina ya ajabu ili watu wapate faida kubwa

emu-three said...

Tatizo kubwa mambo mengi yamekaa kibiashara-biashara, au tuseme kufa-kufaana. Hivi unafikiri malaria ikiisha watu wataishije, dawa, vyandarua nk, vitanunuliwa na nani.
Niliwaza sana kwanini nchi nyingine malaria ni hadithi, wameidhibiti, na mtu akiumwa ni mara chache, ina maana hakuna mbu?
`KINGA NI BORA KULIKO DAWA' hii ndiyo njia pekee ya kutokomeza hili janga, tupambane na mazalia ya mbu,...kuna kipindi serikali au jumuia gani sijui walikuwa wakipita na kupulizia madawa ya kuua vimelea vya mbu, wanapiga kwenye miti, mabwawa, na vyooni...ikaja ikaanza kutiwa maji, ikaja ukitaka mpaka utoe chochote...sasa hakuna tena!
Jamani , jamani hivi sasa watu wapo radhi wengine wafe ili wafaidike...angalia vita vingi Afrika, ukichunguza kuna mikono ya watu wakubwa, wauza silaha...kusipokuwa na vita, viwanda vya silaha vitakufa...kusipokuwa na vita nchi nyingine zitatajirika na kuwa taifa kubwa, na taifa kubwa linatakiwa liwe moja...
Mwenye akili haambiwi tazama..`malaria haikubaliki' ni slogan ya kibiashara...AU NIMEKOSEA!
Pole sana mkuu, twakuombea upone maana nafasi yako kwenye mapigano ipo wazi, watapenya maadui!