Tuesday, May 3, 2011

mwaka mwingine tangu Munga aache mwili

umepita mwaka tangu yule mwalimu wangu wa utambuzi alipoondoka kwenye mwili wake kwa hiari. ilikuwa ni tarehe moja mwezi wa tano 2008.

siku zinasogea na sasa ni mwaka tena

aliniondoa katika ulimwengu wa kutojitambua na kuniigiza katika ulimwengu mpya wa kujitambua. maarifa yake nitayaishi milele. niko huru kwa sababu ya mafundisho yake

migogoro ya kifamilia, mambo ya kiuchumi, propaganda za dini nk, naweza kuvikabili kwa sababu ya maarifa ya huyu bwana aliyenihangaikia na kunijaza maarifa haya

nitamkumbuka milele bwana tehenani aliyenijulisha kuwa mimi ni zaidi ya mwili, kuwa mimi nimekamilika. napaswa kujipenda, kujithamini na kuishi vile nipendavyo bila kuogopa sana jamii ina maoni gani.

asante Munga Tehenan, huko ulikoibukia (reincarnate) uendeleze ngwe hii

3 comments:

emu-three said...

Mungu amlaze mahala pema peponi natumai sasa anafaidi juhudi zake, kwani ki-mani tunaziita hizo juhudi kuwa ni sadaka zenye kuendelea.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

AMEN

SIMON KITURURU said...

R.I.P Munga!