Friday, May 6, 2011

Naulizwa nimejiandaaje na pasaka?

Ni jumamosi moja ambayo ikiisha ni sikukuu ya pasaka (kikristo zaidi). Nakutana na mzee mmoja, mtu mzima waswahili wanasema mwenye heshima zake. Baada ya kumwambia shika-moo, ananiuliza vipi maandalizi ya pasaka?

Nashangaa. Hivi kweli mimi nahitaji kuwa na maandalizi ya pasaka? Eti mkijiandaaga na pasaka huwa mnafanya nini? Ni vitu gain mnaviandaaga? Kweli nahitaji kufanya mandalizi yoyote ya pasaka??

Basi namjibu mzee, sinamaadalizi yoyote, pasaka ije vile itakavyoyenyewe kuja. Sina haja ya maandalizi. Kama ni pasaka kivyake. Misimamo hii imeniweka huru, sina pilika pilika za hapa na pale. Najiona huru zaidi katika hili

1 comment:

Goodman Manyanya Phiri said...

Mzee mwenyewe anaifurahia mno Pasaka hio; lakini ukimchungulia kwa undani, hana hata huo uKrestu wenyewe bali anajitafutia tu matamu ya sikukuu!