Tuesday, May 31, 2011

ustaarabu ni utumwana ushenzi ni uhuru

sijui kuna tofauti gani kati ya ustaarabu na ushenzi. eti ustaarabu ni mbele ya watu na ushenzi ni ukiwa peke yako. kama hii ni kweli basi sisi sote ni wastaarabu (kwa kupenda au kalazimishwa) na pia ni washenzi tuwapo peke yetu.

ila sasa mimi sina taratibu maalumu, sioni kama kuna ustaarabu na ushenzi naona maisha tu yanaendelea.

nikiwa peke yangu home huwa napenda kuwa huru, kuliko na watu wengine. kuna wakati unatembea pekee njiani, unataka uhuru, kaushuzi kakija, unaangalia mbele, unaangalia nyuma, huoni mtu asije kukuona mshenzi, then unaachia, bwaaaaaaaaaaaaa au puuuuuuuuuuuuuuu. bado wewe ni mstaarabu. usiombe ushuzi ukutoroke mbele ya baba/mama mkwe! we mshenzi mkubwa, utatembea umeangalia chini, aibu

ukiwa mkweli na kuwakwepa wale usiotaka kero zao unaonekana mshenzi hata kama ni wazazi, basi unalazimika kuwa karibu nao ili uonekane mstaarabu japo unaumizwa na ukaribu huo! acha utumwa kuwa mshenzi kidogo bwana ili uwe huru usifungwe na ustaarabu

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hivi umesema maana ya ustaarabu ni nini na ushenzi ni nini?..... labda ngoja nirudi kusoma tena:-)

emu-three said...

Ustaarabu wa huyu unaweza ukawa ushenzi wa yule na kinyume chake. Yote yanategemea jamii uishiyo na mahala ulipo kwa mfano yale ufanyayo chooni huwezi kuyafanya hadharani.

Goodman Manyanya Phiri said...

Ustaarabu ni moja tu kwa kila binadamu (labda tutofautiane kwa desturi tu za ule ustaarabu).


Vilevile, ushenzi ni kitu kingine tofauti lakini kimoja hivyohivyo mawazoni ya binadamu kotekote duniani.


Tofauti katika ustaarabu na ushenzi ni usiri: yaani kama nyie hamjamgundua Bwana Phiri kama mshenzi na mlawatu basi naye Phiri ni mstaarabu tu kama "kawa"!


Nje kidogo ya tundu: NDIO MAANA WASHENZI WENGI WANAKIMBILIA MISIKITINI NA MAKANISANI ILI KUZIBA KABISA USHENZI WAO WASIFIKIRIWE HATA KIDOGO!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wewe emu-three, mwanangu anafanya yale uyafanyayo chooni hadharani na bado anaonekana mstaarabu

SIMON KITURURU said...

Mmmmh!

Nimekunukuu hii ndude KWENYE BAADHI,...

...hasa kwenye mndude,...
... kwenye blog posti yangu ile :

``Jela kuna kitu kuwa INSTITUTIONALIZED!´´ ...
kama ulistukia ,...
au kama bado unanitembelea kijiweni kwangu kwa kuwa nimestukia wadau wengi wamesitisha hilo jambo!:-(