Monday, May 16, 2011

wanaotoa Tunzo za bloggers na watoe kwa wawatoleao

nchi ya kitu kidogo, nchi ya kishikaji watu wanatumia miradi ya wengine kufanya kile wanachofikiri wanaweza kukifanya wapendavyo, watakavyo na wawezavyo. serikali daima huwa inawaletea miradi ya wananchi badala ya miradi kutoka kwa wananchi.


mimi kama blogger, ghafra naona eti kuna bloggers awards. sijui blogu yangu imo au haimo. ni dili za wajanja kwa kutumia umma wa bloggers, kwa kushirikiana na bloggers rafiki zao na kwa kutunga vijiblog vya kupatia awards.


sasa wamegroup bloggs vile waonavyo wao ndivyo visitahirivyo awards na sio kiuhalisia. blog mpya zimeshika nafasi nyingi za awards, sijui ni watu gani walikaa na kuamua walivyoamua. ni awards, ni tunzo 'kwetu ma-bloggers' japo kuwa hatujui hasa ni nani kapangilia na kuamua kutoa hizo tunzo.


blog kama yangu, ni ya mawazo huru na mitizamo mipya (upande mwingine) haina nafasi. hivi blog ya Matondo kwa mfano yenye kufundisha kiswahili , fikra za ijumaa nk, utaiweka upande gani? hivi kijana wa changamoto anafaa award ipi?

binti ruhuwiko na koero je, hadith, story, au kuwakemea wanaume dhidi ya wanawake? sijaona award ya kaluse au utambuzi na wala ya kijjin kwa chacha

na watoe wapendavyo. infwakti, kwangu ikija award hata iwe ya uongo, nitakikaribisha, isipokuja haitoathiri uamuzi wangu wa kublogu.

lakini huyu aliyeamua kutoa award na ajitambulishe yeyeni nani kwanini kaamua kutoa hizi award na yuko wapi. sio kufanya mambo nyuma ya pazia kwa jina la bloggers

3 comments:

Mcharia said...

http://mtayarishaji.blogspot.com/2011/05/majibu-ya-mmiliki-wa-tuzo-za-blog.html

Mzee wa Changamoto said...

Kaka nashukuru kwa kuliona hilo. Nashukuru kwa jitihada za kuelimisha na kuweka bayana.
Ninalowaza zaidi ni kuwa KWANINI MTOA TUZO HAJULIKANI NI NANI NA ANAKAA WAPI?
Kwanini wanaotoa maoni wawe Anonys pekee? (nahisi ni yeye mwenyewe anayekuja na maoni ya sifa)
Kwanini TUZO ZITEULIWE NA WATU WASIOJULIKANA? Katika majibu yake kwangu amesema "Na unavyosema sijui tuwaandikie watu watueleze blog zao zinahusu nini. Kwa taaarifa yako kuna watu wengi wanablog lakini hawajui hata blog zao zinaelekea wapi. Kuna maswali tumetuna na kuna wengi wamesharudisha lakini nakwambia ni kama 50% ya waliorudisha mpaka sasa hivi hawajui blog zao zinahusu nini au wasomaji wa blog zao ni nani."
HAPA NDIPO NINAPOWAZA kuwa KAMA MTU HAJUI ANAANDIKA KUHUSU NINI, NA ANAMUANDIKIA NANI, NI KWANINI AWE NA TUZO?
Kama ulivyosema kwenye Facebook....HII NI BIASHARA

emu-three said...

Tuwenii macho na vitu kama hivi, sidhani kuwa tulianzisha blog zetu ili tupate hizo zawadi.
Ok, labda ni tuzo, na kama ni tuzo, hawo waandaji wapo wapi, na ni akina nani, na masharti au vigezoo vya hizoo tuzo ni vipi
Tuelewe kuwa nyanja hii ya mawasiliano imegubikwa na sintofahamu nyingi, wapo ambao kila kukicha wanabuni mbinu za kupata kwa kutumia migongo ya watu.
Hatuna uhakika na hili, kama lipo na watu wana nia njema, waweke wazi, sio mbaya mkawajali wanablog...cha msingi mjue kuwa wengi wa wanablog ni wapiganaji kwa ajili ya manufaa ya jamii, sio kwa ajili ya biashara au zawadi, kama zipo tutashukuru, sio mbaya.