Tuesday, June 14, 2011

fahari ya kuishi na kutembea mitaani Dar, kula kula


baada ya kuzunguka mitaa kibao ya Dar kwa miguu na kwa dala dala sasa nimeona tofauti ya mji huu na nimeona kile ninachokikosa kwa kutokuwa Dar. kwanza zamu hii hamna joto kabisa lakini ishu ni kula kula vyakula vya asili. Dar na wachuuzi wengi na wafanya biashara. kwa mfano, kona hii wanachoma mahindi, unajichukulia mmoja unamung'unya, kona ile wana miwa, imeandaliwa unatafuna. kuna ile wanachua chungwa, unakunja sura na kupanua domo huku hukilishindilia likamuliwe mdomoni. kona nyingine wanauza mihogo ya kuchoma kama sio viazi. ulaji wa hivi ndo naukosa kwa kuwa nje ya Dar, saa za foleni lazima utafune kitu tu

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kula kula, haya Kamala we tamanisha tu ila muda si mwingi nami nitakuwa nakulakula vya asili:-)

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

safi

Goodman Manyanya Phiri said...

Kamala umezidi kula nawe! Sasa watoto watakula nini?

ANYWAY, unigawie nami hayo mahindi ya kuchoma. Napenda sana!

SIMON KITURURU said...

Jamani!:-(