Wednesday, June 29, 2011

NILIDHANI NINGEPATA MUDA WA KUTOSHA KUWA KIJIWENI

hiki ni kijiwe, kama mnavyojua huwa tunasogea vijiweni baada ya kazi kupata umbeya, kuchati na kunywa au kula hiki na kile na kwa hiyo ndo huwa nafanya hivyo hapa kijiweni kwetu

lakini hali imekuwa tofauti, najikuta niko bize kuliko wakati mwingine wowote baada ya kubadilisha mfumo wangu wamaisha ili pamoja na mambo mengine niweze kuwa kijiweni. nimejimilikisha vifaa vya kisasa vya TEHAMA, nikawa karibu na mtandao na nini sijui

ghfara nilivyotarajia sivyo, najikuta siwezi kupata hata dakika chache za kuwepo kijiweni,lakini natumaini kuanzia leo ni non stop. ni kublogu kwa kwenda mbele au unaonaje? hata mwanzoni wakati nabadili life style nilifikiria hivi lakini haikuwa hivyo

lalbda sasa itakuwa?

2 comments:

SIMON KITURURU said...

Mara nyingi kufikiria hivi huwa haiwi hivyo,...
... kwa kuwa siye ni BINADAMU ambao moja ya udhaifu wetu ni kuona picha nzima kinusunusu!:-(

emu-three said...

Kwelii mkuu, unaweza ukawa na mawazo mengiii, sasa shika kalamu, sasa shika laptop, sasa anza kuandika, unajikuta umeandika `kiduchu' muda hautoshi, majukumu ndio usiombe na huku bongo, ndio akabisa..kwani umeshika kalamu, unasikia aaaah, umeme umeenda kwao, ukatafute mshumaa,m dukani ukirudi...ooh, kuna mgeni aaah, kuna hili, siku imeisha..ukifika ofisini, oooh, kazzi nyingi,unasema nikirudi home nitaandika...oooh, njiani folenii unakaaa, au umesimama masaa matatu hadi manne, utafikiri unaenda mikoni...oh, jamani ...jamani..nilidhani ningepata muda, wa kutosha, ...lakini wapiiii!