Thursday, June 16, 2011

nitaamia heyateli tu, voda ni noma

najiuliza kama mimi sio chizi kwa mtizamo wa vodacom, niliwapigia simu kuwaelezea ya kuwa mkoa wa kagera unashida saana za kimtandao wao. jamaa akanibishia na kuniambia kuwa uko sawa, nikamwambia nakaa maeneo kadhaa ya mkoa wa kagera lakini mtandao wao unanizingua, akanikatalia kuwa hapa na uko sahihi

nyumbani kwangu nalazimika kuacha simu dirishani, nina makazi mengine huko ndo usiseme, juu ya mti na kwenye kimori, lakini jamaa wa voda wananibishia nakudai kuwa tatizo ni simu yangu, nina simu zaidi ya moja, na majirani nao walalamika, kweli tatizo ni hilo?

kubwa zaidi anayeniambia hivyo yuko dar mimi niko bk, yawezekana mimi ni chizi kwa malalamiko hayo?

hakiyanani nitaamia heyateli tena weekend hii

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

kama ndo hivi hakuna haja ya kuwa na simu wakati mtu huwezi hata kutulia nyumbani kwako na kuongea na marafiki kwa utulivu. Tatizo hilo tulilipata au tulikumbana nalo pia katika nyumba yetu Songea yaani hatukuweza kuongea na simu ndani ya nyumba mpaka tutoke nje ya nje ya nyumba tulikuwa tukitumia Zain sijui ndio hiyo "heyateli" uisemayo Kamala" kaaazi kwelikweli...

chib said...

Voda wajinga, wengine wanapo pokea kero za wateja wanatafuta namna ya kuzitatua, lakini hao mafisadi wanakataa

Goodman Manyanya Phiri said...

Hata ingekuwa ni simu yako pekee yenye matatizo, Mkuu Kamala, Voda hawanahaki ya kukujibu hovyo. Waombe majirani zako nao wawapigie simu na wakiendelea na kujibu pumba mimi napendekeza tuanze kuwapiga vita hapa hapa mtandaoni wakome kabisa na waihame nchi kama ikibidi, kwani [ya Mteja Kamala daima ni sahihi]! Na huo ndio msemo waliyoanzisha wenyewe wafanyabiashara!

Mcharia said...

JE WAJUA? KUNA NAMBA SITA TATU KATIKA NEMBO YA VODAPHONE (666), unaweza kuziona? JE WAJUA? nembo hii ya vodaphone inafanana kwa karibu kabisa na nembo ya kundi maarufu la Ku Klux Klan (KKK) la marekani?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mcharia sijawahi onae, nisaidie nitaionaje hiyo?