Friday, July 8, 2011

katika kutafuta ubingwa waweza jihisi sio bingwa

m-blogu simon kitururu anadai ya kuwa kuna ubingwa mwingi na labda yuko sahihi. anasema yawezekana wewe ni bingwa wa kutongoza japo kuwa hamna mashindano hayo, kuna bingwa wa kunaniliihino, bingwa wa kuchamba na hata bingwa wa kupenga

kama haitoshi kuna hata bingwa kubana ushuzi. yaani mtu unakaa namwenzio nyumbani au ofisini miaka lukkuki, hujawahi sikia hata siku moja shuzi likimtoroka, huyu ni bingwa japo kuwa uhalali wa ubingwa wake nautilia shaka kwani ushhuzi upo ili ubwaguliwe na sio kubanwa.

kuna hata bingwa wa kula chakula na kukimaliza kwenye sahani, bingwa wa kuangalia jicho baya na hata bingwa wa kushangaa. ubingwa uko mwingi.

ebu jiangalie katika maisha ya kawaida ya kutetea ubingwa wako huo wa siri.
nikipendacho kuhusu mimi basi huwa ni ubingwa wangu juu ya hasira, basi mimi najua kuibana hasira isinitoroke ili nije kujuta baadaye.

eti wewe una ubingwa gani usio shindaniwa au wa siri? kula? kujisaidia? kuoga uchi wa mnyama au?
samahani, wazo liko kiwaluwalu

No comments: