Wednesday, July 20, 2011

kumbe mimi ni msomi!

Japokuwa sina elimu kubwa ya dunia hii name naitwa msomi. Kuna jamaa mmoja mfanyabiashara anayependelea kuniita msomi. Binafsi sipendiagi kuitwa au kutambulishwa kwa cheo chochote kila katka jamii yoyote ile, huwa napendaga tu kuitwa binadamu au mtu au angalau kwa majina ya kibabe na kimagharibi niliyopewa na wazazi wangu

Sasa mfanya biashara huyu anapendelea kunitaja kama msomi katika mazungumzo yoyote yale tuzungumzayo. Mimi nambishia na kumwambia kuwa ni mtu kama wewe, anakataa nakusema kuwa mimi ni muelewa namsomi!

Ehh anadhibitisha usemi wake, anadai niingiapo dukani kwake nakukuta bidhaa auzazo kama vile mchele, huwa naulizia huu mchele ni wa wapi,, shinyanga, gaita au mwanza? Pia huwa napenda kujua mifumo mbali mbali ya bidhaa zake, aina na jinsi zilivyo na kwa nini zilivyo. Anadai nafanya hivyo kwa kuwa mimi ni msomi kwani tangu aanze biashara, wateja wengine huwa hawaulizi maswali haya, wao hununua tu na kuondoka na kwa hiyo mimi ni msomi!

Nikaishiwa hoja nakumwacha aendelee kunitambulisha kama msomi

KUMBE MIMI NI MSOMI!

2 comments:

SIMON KITURURU said...

Wewe ni Msomi hata mimi hilo nimestukia!:-(

emu-three said...

Mkuu wewe ni MTHOMI...Nakumbuka siku fulani nyuma nikiwa kidato cha sita, nilikwenda kijijini kwa likizo, kukawa na basi limeharibika, mara bibi yangu akanijia na kuniambia kuwa kuna basi limeharibika hapo mbele niende nikasaidie kulitengeneza, nikabakia mdomo wazi, mimi nasomea biashara wapi na wapi mambo ya magari
'Bibi mimi sio mtaalamu wa kutengeneza magari' nikamwambia
'Wewe msomi mnzima huwezi kutengeneza gari, sasa unafuata nini shule, sisi tulitarai ukirudi likizo kila kitu kikiharibika tunakuita wewe...'