Wednesday, July 27, 2011

mtoto hamilikiwi na wazazi wake, anajimiliki mwenyewe

anajimiliki huyu
nikaingia katika mijadala ya kibinadamu ya kutaka kumiliki hata tusivyo vihitaji. sasa jamaa wanajadili nani anamiliki mtoto kati ya wazazi wake yaani baba na mama? wanaume wanadai ni baba na wanawake wanadai ni mama. mwanamke mmoja aliyekulia katika mfumo dume anadai ni baba nikaulizwa mimi, nilishangaa, kwa nini asimilikiwe na wazazi wote wawili yaani baba na mama? lakini je, sisi twaweza kumiliki mtu au kumiliki chocote duniani? hapana.

basi kila mtu anajimiliki tu! hakuna aliyeomba kuzaliwa, kuzaa ni matokeo ya mihemko ya kihisia na kwa hiyo tumzaaye anajimiliki hata kama tuna jukumu adhimu la kufanyia yaliiyomema mpaka atakaposimama mwenyewe.


ili tuzaliwe, tunaanzia maisha kwenye tumbo la mwanamke, tukizaliwa tunaula mwili wa mwanamke, then tukikua tunamhitaji dada, then girlfriend then wife! kwa mtu aliyeoa kama mimi, nahitaji mke wangu kuliko mtu yeyote yule hata hivyo mtoto anajimiliki yeye mwenyewe bila kumilikiwa na njia iliyomleta duniani (wazazi) kwani ile ni njia tu ya kuingilia duniani

1 comment:

Goodman Manyanya Phiri said...

Hata yeye mwenyewe hawezi kujimiliki, Mkuu, apende asipopenda.

Dunia ndio itammiliki kutokana na urithi, malezi aliepata,lishe iliejenga akili na mwili wake, kisha mahitaji ya jamii.

Mfano Kama huko anakoishi panavita, hakika ataona rahisi kuwa askari kuliko karani; na kama anaishi sehemu yenye biashara ya madawa ya kulevya, jamii itamiliki hizo akili zake nyingi katika biashara hiyo haramu zaidi kuliko vile angekuwa daktari.