Friday, July 1, 2011

Ndoa si ndoano, bali dili, mpango mwema


Mimi naonelea na kufikiria ya kuwa ndoa ni kitu kizuri sana, nasema ndoa ni dili, ni mpango mwema. Naifagilia lakini kwa wakati sahihi, pahala sahihi na mwenza sahihi. Ila sasa, niongeapo na wanandoa kama mimi, huwa napata majibu tofauti, ya ajabu, ya kupendeza na labdda mengine ni ya kushtukiza.


Eti wewe huwa una siri na mwenza wako wa ndoa? Eti kuna vitu unavijua yeye havijui? Kwamfano, unakuta mwanandoa mambo ya fedha ni siri. Mume haujia mke anamiliki pesa kiasi gani na mke pia hajui, mambo ya amana ni siri kabisa, wanakopeshana na kudaiana, naona kama hii sio sahihi na niseme labda haiwezekani fulani.


Wakati mwingine wanandoa hawajui mwenzao anafanya kazi gania ua wapi au kasafiri kwenda wapi, wakutana tu kitandani the asubuhi kila mtu lwake.


Kuna ndoa moja nimeshuhudia jamaa wanaishi nyumba moja na kulala vyumba tofauti japo mara moja moja hukutana kitanda kimoja, au kwa kifupi kuna baadhi ya ndoa ziliisha vunjika zamani japo wanaogopa kuzivunja rasmi kwa kuogopa umbea wa jamii itasema nini juu yao au kwa eti kulinda heshima kwa wazazi!!! Maweeeeeeeee


Hivi kuna siri kweli katika ndoa?


Ndoa nyingine huingiliwa na kuendeshwa na wazazi na ndugu wa mwanaume, kama unataka kudumu katika ndoa na unampenda mkewe, punguza spidi ya ndugu jamaa na marafiki, wewe fanya mkea kuwa msaidizi wako mkuu au hata mtendaji, mambo yote yahusuyo nduguzo na mamako, yasiletwe kwako moja kwa moja bali ni shart yapitie kwa mkeo kwanza na usisikilize umbea wa moja kwa moja, hii itaondoa unafiki na kujipendelea na nduguzo kumwomea mkeo wivu.


Kumbuka binadamu tunahitajiana, na kuhitajiana kukuu ni kwenye ndoa, ni kwa mke na Mume ni katika upendo halisi na wa kweli. Tuna upendo wa kupeana, tuna hisia za kupeana, tuna mihemko, nk vya kupeana,


Bado naamini ndoa si ndoano na ni uchaguzi sahihi kwa mke / mume kuingia kwenye ndnoa. Furahia ndoa yako mkuu au vp?

1 comment:

emu-three said...

Kweli mkuu ndoa kama ndoa sio ndoana, bali wanandoa ndio wanaofanya ndoa iwe sivyo ndivyo...cha msingi ni kujua misingi ya ndoa,kabla ya kuingia ndani ya ndoa....mara nyingi najiuliza, ukitaka kuwa dakitari unausomea udakitari, ukitaka kuwa mwalimi unausomea ualimu...au sio, lakini ukitaka kuwa mwanandoa unakurupuka tuuu, unafikiri matokea yake yatakuwaje , kama sio kutolewa nishai! Kila kitu kinahitaji shula baba, hata kula huwezi kula tu, mpaka ujue jinsi gani ya kuutoa mkono na kuupeleka kinywani, vinginevyo utaweka puani!