Monday, July 25, 2011

wakazi wa vijijini Tanzania ni daraja la pili?

mipango mingi ya maedeleo nchi hii huwa ni ya mijini. mipango mikubwa na mikutano hufdanyika mijini kwa kiasi kikubwa, nini tatizo la wakazi wa vijijini> umeme uko mijini, huduma za maji hutolewa vijijini na kupelekwa mijini! sherehe za kitaifa hufanyika mijini

miji ya Dar, Arusha na mwanza kama sio dodoma hupewa sana kipaumbele. maonyesho na hafra kibao hufanyika kwenye miji hii. hata ikiwa ni nje ya miji hiyo, basi mambo huwa ni mijini, wao huita makao makuu ya mkoa kama sio wilaya.

hivi wanavijiji wamekosea nini? hata kwenye ajira, wanaajiri zaidi watu wa dar na miji ya karibu nayo. kazi za serikali na mashirika yake, mabenk, makampuni nk ajira huwa ni Dar na miji mikubwa wao wanaita makao makuu! usaili hufanyika kwenye miji mikubwa, ukiitwa usailini, ukahesabu gharama za kufika pale harafu huna uhakika wa kupata kazi, unakaa pembeni, unaachana nayo wanaajiriwa wa mijini na kuletwa huku uliko kwa kazi unayoweza

huduma kama za maji na umeme huzalishwa vijijini lakini hupelekwa mijini wananchi wa vijijini hubaki kufurahia mingurumo ya machine, kuona nyaya na mabomba yakipitisha huduma nakwenda mijni, kila sera iko kimiji miji tu. tunaambiwa tusiharibu mazingira ili kutunza vyanzo vya maji ili watu wa mijini wapatemaji huko wa vijijini wakibakia kushangaa na kusubila mvua ziisizo na uhakika!

hata bodi za mazao ya vyakula hukaa mijini na kuwakamua wakulima wakati wa misimu tu. bara bara za vijijini hulimwa kwa mikono! japokuwa kodi hufautwa mpaka vijijni
tuna madaraja? je sisi wakazi wa vijijini tnatofauti gani na wale wa mjini

No comments: