Tuesday, July 12, 2011

wazazi wanapotaka kukupangia maisha!

wanadai eti wazazi ndo Mungu wako wa duniani, lakini je uko tayari wazazi wako waingilie masiha yako na kukutawala wakupangie cha kufanya hata kukuchagulia mke/mume?

eti nikweli kuna laana ya wazazi? wahaya wanatamaduni eti dume zima kama mimi lenye familia likienda kinyuma na atakavyo mzazi, basi mzazi aweza nilaza chini na kunitwanga mijeredi kadhaa, eti wewe unaweza kubali kutandikwa na wazazi wako awe baba mama, mjomba au hata shangazi?

kwanza mimi silaaniki na wala silaani, mtu yeyote anayejiona anaweza kunirushia laana kapotea

then mzazi wangu yeyote asijejiroga kunirekebisha kwa kutumia kiboko, itakuwa kihama kwake, sikimbii wala silali na ole wake anitwange mijeredi ya mgongoni eti aninionya, wewe! nami natafuta kiboko ili asikie utamu wake kwangu, akinitwanga miwili nitalipiza nne

kwa nini mijeredi iwe mitamu na baraka kwa wadogo then iwe mitamu na laana kwa wakubwa?

mtu yeyote asijejiroga, wewe kama unawaamini na kuwaogopa wazazi kivyako mkuu au

No comments: