Tuesday, August 23, 2011

eti wewe unakubali hii juu ya kichwa cha mwanake kama isemavyo bible?

1 Wakorintho 1: 3-10

3 Lakini nataka mjue kwamba kichwa cha kila mwanamume ni Kristo; nacho kichwa cha mwanamke ni mwanamume; nacho kichwa cha Kristo ni Mungu. 4 Kila mwanamume ambaye husali au kutoa unabii akiwa na kitu juu ya kichwa chake hukiaibisha kichwa chake; 5 lakini kila mwanamke ambaye husali au kutoa unabii kichwa chake kikiwa hakijafunikwa hukiaibisha kichwa chake, kwa maana ni kana kwamba yeye ni mwanamke mwenye kichwa kilichonyolewa. 6 Kwa maana ikiwa mwanamke hajifuniki, na akatwe nywele pia; lakini ikiwa inafedhehesha kwa mwanamke kukatwa nywele au kunyolewa, basi na afunikwe.

7 Kwa maana mwanamume hapaswi kufunika kichwa chake, kwa kuwa yeye ni mfano na utukufu wa Mungu; lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume. 8 Kwa maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke alitoka katika mwanamume; 9 na, zaidi ya hayo, mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume. 10 Ndiyo sababu mwanamke anapaswa kuwa na ishara ya mamlaka juu ya kichwa chake kwa sababu ya malaika.