Thursday, August 4, 2011

"wazee wa miaka 70 wasipige kura"

katika mkutano juu ya ushiriki wa vijana katika uundwaji wa katiba mpya ya tanzania, nilifurahia mtizamo wa msemaji mmoja aliyedai kuwepo na ukomo wa umri wa kupiga kura kama kuna mwanzo

jamaa anadai busara iliyotumika kuamua vijana chini ya miaka 18 wasipige kura then hiyo hiyo itumike kuamua wazee wasipige kura pia na akaweka pendekezo la kuwa mika 70 na kuendelea wasipige kura

hii imetulia kwa nini vijana chini ya 18 wasipige kura then wazee wapige? unawezaje kuchagua mambo ya kesho wakati kesho yenyewe hautakuwepo?

imetulia na iingizwe kwenye katiba

1 comment:

Goodman Manyanya Phiri said...

Kusema miaka 18 kama kipimo ni utumbo uliohalalishwa bure tu; bora miaka 10 au 9 kwani wengine tayari wanazaa watoto kwa umri hiyo na wengine tayari ni wapigania-uhuru katika umri huo kama Julius Malema alivyoanza (Miaka 9) Afrika Kusini.


Vilevile mawazo ya kwamba mtu akiwa na 70 "amekwisha" hayana misingi. Mbona hata ukiwa na 30 unaweza ukapiga kura saa nane, na saa tisa njiani kwelekea nyumbani ukagongwa na gari ukafa?